Tuesday, May 13, 2014

UBINAFSISHAJI VIWANDA VYA NGOZI UMEATHIRI UCHUMI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dk. Titus Kamani
 
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dk. Titus Kamani, amesema tangu serikali ilipobinafsisha viwanda vya usindikaji wa ngozi, kiwango cha uzalishaji wa bidhaa hiyo kimeshuka kwa kimeshuka kwa kiasi kikubwa.
Dk. Kamani aliyasema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau wa tasnia ya ngozi uliofanyika jana  jijini Dar es Salam.

Alisema licha ya Tanzania kuwa nchi ya pili  uwingi wa mifugo barani Afrika baada ya Ethiopia kwa kuwa na ng`ombe milioni 22.8, mbuzi 15.6 na kondoo 7.0,  lakini  kipato kinachopatikana kutokana na bidhaa  ya ngozi ya mifugo hiyo hailingani na idadi ya mifugo iliyopo.

Alisema  kwa  utafiti wa mwaka 2013 uzalishaji wa vipande vya  ngozi ya Ng`ombe umeshuka kutoka milioni 3.4 hadi 2.9, Mbuzi 4.4 hadi 3.6 na Kondoo milioni  2.0 hadi 700,000.

Alitaja  sababu  kubwa  zinazochangia  sababu  kubwa inayochangia uzalishaji wa ngozi ni kutokana na kutokuwa na viwanda vya kutosha vya usindikaji wa ngozi pamoja na utoroshaji wa ngozi kwenda katika jirani kupitia njia za panya.

Aidha, alisema kuwa serikali inajipanga kuhakikisha shughuli  za uzalishaji  na  usindikaji  wa bidhaa hiyo zinafanyika hapa hapa nchini kuanzia hatua ya awali mpaka ya mwisho, ili kuhakikisha  taifa linanufaika kiuchumi tofauti na ilivyyo sasa.

Alisema mpaka sasa uzalishaji  unaofanyika nchini  unaishia  katika hatua ya awali tu ya wet bluu,  ambayo haina faida yeyote.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment