Monday, May 5, 2014

WABUNGE KUCHANGIA DAKIKA SABA TU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Wabunge wa Bunge la Bajeti linaloanza kesho mjini Dodoma, wamepunguziwa muda zaidi wa kuchangia kutoka dakika 15 hadi saba.
Bunge hilo la Bajeti limetengewa siku chache ambazo zitalilazimu kuendeshwa kwa kasi ili kukamilisha shughuli zake.
Habari zilizopatikana jana zilisema hatua hiyo inatokana na muda kuwa mfupi kwa kuwa Bunge hilo litakutana kwa siku 52 ikiwa ni pungufu ya siku 28 ikilinganishwa na mkutano kama huo wa mwaka jana.
Katibu wa Bunge, Thomas Kashililah alipoulizwa kuhusu taarifa hiyo jana alisema ofisa habari wa Bunge, Owen Mwandumbya angeweza kulizungumzia. Hata hivyo, Mwandumbya alipoulizwa alisema atazungumza leo.
Miongoni mwa marekebisho yaliyopitishwa katika kupunguza muda wa vikao ni pamoja na kuendelea kufanyika hadi Jumamosi pia kumalizika saa 2:00 usiku.
Ratiba iliyotolewa na Bunge imesema utaratibu wa sasa unalilazimisha lifanye uamuzi wake (kupitisha au kutokupitisha), Bajeti ya Serikali pamoja na Sheria za Fedha ifikapo mwishoni mwa Juni kila mwaka, ili kuruhusu utekelezaji wa bajeti husika kuanza Julai Mosi, siku ya kwanza ya mwaka mpya wa fedha.
Chanzo:Mwananchi

No comments:

Post a Comment