Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wakazi wa Ukonga wameamua kujitolea kujenga daraja la muda eneo
la Mongolandege baada ya lile la awali kusombwa na mafuriko kutokana na
mvua za masika zinazoendelea kunyesha na kusababisha kukatika kwa
mawasiliano ya barabara maeneo hayo.
Ujenzi wa daraja hilo la muda umeshaanza, lengo ni
kuhakikisha daraja hilo linatumiwa na waenda kwa miguu na bodaboda ili
kuwapunguzia adha ya kuzunguka umbali mrefu hali ambayo imekuwa kero kwa
wakazi na inawaongezea gharama za maisha.
Mbunge wa jimbo hilo, Eugene Mwaiposa alikiri
kufahamu tatizo hilo na aliishawasiliana na mamlaka zinazohusika kwa
ajili ya kupatia ufumbuzi tatizo hilo na kwamba ana imani kuwa bajeti
ijayo itakuwa na fedha za ujenzi wa daraja hilo.
“Nimewasiliana na mamlaka husika na pengine katika
bajeti ijayo litakuwapo fungu la ujenzi wa daraja hilo,” alisema na
kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kuwa wavumilivu kipindi hiki wakati
mchakato wa ujenzi unafanyika.Ujenzi huo wa daraja la muda unafanywa kwa
pamoja baina ya wakazi na waendesha bodaboda wa eneo hilo na mtabibu wa
tiba za jadi, Dk Abdallah Mandai, ambaye ametoa Sh1 milioni kusaidia
ujenzi huo.
“Nimewapa fedha kusaidia ujenzi wa daraja ili walau waenda kwa miguu na pikipiki wapite,” alisema.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
No comments:
Post a Comment