Home » » WANANCHI WAJITOLEA KUJENGA DARAJA

WANANCHI WAJITOLEA KUJENGA DARAJA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Wakazi wa Ukonga wameamua kujitolea kujenga daraja la muda eneo la Mongolandege baada ya lile la awali kusombwa na mafuriko kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara maeneo hayo.
Ujenzi wa daraja hilo la muda umeshaanza, lengo ni kuhakikisha daraja hilo linatumiwa na waenda kwa miguu na bodaboda ili kuwapunguzia adha ya kuzunguka umbali mrefu hali ambayo imekuwa kero kwa wakazi na inawaongezea gharama za maisha.
Mbunge wa jimbo hilo, Eugene Mwaiposa alikiri kufahamu tatizo hilo na aliishawasiliana na mamlaka zinazohusika kwa ajili ya kupatia ufumbuzi tatizo hilo na kwamba ana imani kuwa bajeti ijayo itakuwa na fedha za ujenzi wa daraja hilo.
“Nimewasiliana na mamlaka husika na pengine katika bajeti ijayo litakuwapo fungu la ujenzi wa daraja hilo,” alisema na kuongeza kuwa wananchi wanapaswa kuwa wavumilivu kipindi hiki wakati mchakato wa ujenzi unafanyika.Ujenzi huo wa daraja la muda unafanywa kwa pamoja baina ya wakazi na waendesha bodaboda wa eneo hilo na mtabibu wa tiba za jadi, Dk Abdallah Mandai, ambaye ametoa Sh1 milioni kusaidia ujenzi huo.
“Nimewapa fedha kusaidia ujenzi wa daraja ili walau waenda kwa miguu na pikipiki wapite,” alisema.
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa