Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais Jakaya Kikwete amezitaka taasisi binafsi kushirikiana na
Serikali katika kampeni ya kutokomeza maambukizi mapya ya virusi vya
ukimwi nchini.
Akizindua kampeni ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa
ajili ya kuchangisha Sh 1.5 bilioni zitakazotumika kusaidia kutokemeza
maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vitokanavyo na ukimwi, Rais Kikwete
alisema Ukimwi bado ni tishio.
Rais Kikwete alisema licha ya kwamba maambukizi
mapya yamepungua kwa asilimia kadhaa ikilinganishwa na miaka iliyopita,
bado jitihada zinahitajika kupambana na ugonjwa huo.
“Lengo la Serikali ni kukomesha maambukizi ya
virusi vya Ukimwi, ingawa peke yetu hatuwezi, hivyo tunahitaji
ushirikiano wa hali na mali kutoka taasisi nyingine za binafsi ili
kufanikisha kampeni hii,” alisema Rais Kikwete.
Katika kampeni hiyo, Tume ya Kudhibiti Ukimwi
(Tacaids) kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM), inatarajia
kukusanya Sh1.5 bilioni zitakazosambazwa mikoa yote ya Tanzania kwa
lengo la kusaidia kupunguza maambukizi mapya.
Mwenyekiti mtendaji wa Tacaids, Fatma Mrisho
alisema zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro litafanyika kwa siku sita
kuanzia Mei 15 na washiriki wataanza kuwasili mjini Moshi Mei 14.
Mrisho alisema lengo la kampeni hiyo ni
kuhakikisha wanapunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) hadi
kufikia asilimia sifuri na kupunguza vifo vitokananyo na ugonjwa huo na
kumaliza unyanyapaa kwa waathirika.
“Kampeni hii inafanyika mwaka wa 13 sasa. Mwaka
jana tulikusanya milioni 700 katika kampeni kama hii. Fedha ambazo
zimesaidia kupunguza mara mbili zaidi,” alisema. ya maambukizi mapya
kulinganisha na miaka ya nyuma,” alisema Mrisho.
Mkurugenzi Mtendaji wa GGM, Michael Van Anen alisema kampeni hiyo itahusisha wananchi kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Anen alisema katika kampeni hiyo watoto wawili wa
kituo cha kulelea watoto yatima cha Moyo wa huruma kilichopo Geita
wataungana na wananchi wengine kupanda mlima Kilimanjaro siku hiyo.
“Tumefanikiwa kuzifikia na kuzisaidia asasi
mbalimbali hapa nchini kupitia kampeni hii ambayo tumekuwa tukifanya na
wadau wengine kama Captal Drill, Wambi Oil, Mantrac, Prime Fuel, African
Barrick Gold, Airtel, Southern Sun, Zara, MACS, Ausdrill na wadau
wengine wanaopenda kuungana kufanikisha kampeni hii pamoja na sisi.
“Tunafanya kampeni kwa lengo la kusaidia kupunguza ukimwi ambao kwa hapa nchi bado ni tishio,” alisema Anen.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment