Home » » WAZIRI:MCT INA KAZI KUBWA YA KUREJESHA HADHI YA HABARI

WAZIRI:MCT INA KAZI KUBWA YA KUREJESHA HADHI YA HABARI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT)Kajubi Mukajanga.
 
Waziri  wa Habari Utalii, Utamaduni na Michezo, Said Ali Mbarouk, amesema Baraza la Habari Tanzania (MCT) lina kazi kubwa ya kuirejesha tasnia ya habari katika hadhi yake.
Akizungumza katika kongamano la siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari visiwani hapa, alisema taifa linathamini na kuheshimu uwapo wa vyombo vya habari kutokana na mchango mkubwa wa ujenzi wa taifa, hivyo wanahabari wanapaswa kuhakikisha tasnia ya habari haitumiwi na wajanja kwa manufaa yao binafsi.

“Angalieni dhima yenu kwa taifa, vyombo vya habari vina majukumu makubwa na mazito, msitoke nje ya mipaka ya uhuru wenu, msikubali kabisa kutumiwa na wanasiasa,” alisema Said.

Aliwataka waandishi wa habari kutumia fursa ya kutetea mambo ya msingi ya tasnia ya habari nchini na kujiepusha kutumiwa na wanasiasa kwa kutumia kivuli cha mabadiliko ya katiba badala yake wautumie uhuru huo kwa kuhubiri amani kwani bila ya amani, uhuru wa vyombo vya habari hauwezi kuwapo.

Alisema kumekuwapo na matatizo makubwa ya kimaadili yanayofanywa na baadhi ya waandishi wa habari kwa kutozingatia umuhimu wa mila na utamaduni.

Alisema taratibu zilizowekwa kisheria kusajili na kusimamia vyombo vya habari hazifuatwi kikamilifu kutokana na kuzorota kwa maadili ya vyombo vya habari na maadili ya waandishi wa habari.

Alisema waandishi wa habari wamekuwa wakinyanyaswa, kudhalilishwa na kunyimwa habari na baadhi ya watendaji kwa kisingizio kwamba wao si wasemaji, wakubwa wao hawapo pamoja na kuwaambia njoo kesho na kuwataka waandishi kutovunjika moyo na hali hiyo.

Akiwasilisha mada katika kongamano hilo, Ali Saleh alisema ana imani kuwa endapo Rasimu ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano ikipita, itafungua milango zaidi ya uhuru wa vyombo vya habari na waandishi wataweza kupata haki zao za msingi.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa