Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Tanzania Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed Fakih akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bi. Agnes Mtawa.
Mh. Balozi akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mh. Balozi akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili mara tu baada ya ziara yake.
*****
*****
Balozi
wa Visiwa vya Comoro nchini Tanzania Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed
Fakih ametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya
kujitambulisha, kuangalia fursa na wigo wa kuanzisha mahusiano mazuri
kati ya nchi yake na Hospitali hii.
Dkt.
Mohammed amesema kuna
Wacomoro wengi ambao wanapata huduma za tiba Hospitalini hapa hivyo
ameona kuna haja na umuhimu wa pekee kuwa na uhusiano wa
kiutendaji rasmi ili Watalaam kutoka Komoro waje kujifunza na kupata
uzoefu wa utoaji huduma za tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.
0 comments:
Post a Comment