Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
BENKI
Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa hadhari kwa wananchi kutambua kuwa kughushi
pamoja na kumiliki fedha bandia kwa nia ya kuzitumia ni kosa la jinai,
linalosababisha mhusika kushtakiwa kwenye vyombo vya sheria.
Imegundulika kwamba
kukosekana elimu kuhusu utunzaji wa noti, kunasababisha kuwepo uchakavu
wa noti hizo katika mzunguko wa fedha hali inayochangia kushuka uchumi
nchini.
Akizungumza na
mwandishi wa habari hizi juzi kwenye viwanja vya Maonesho ya Kimataifa
ya Biashara (Sabasaba), jijini Dar es Salaam, Ofisa Mkuu wa benki hiyo
Idara Kurugenzi za Kibenki, Patrick Fata alisema wanatoa elimu kwa
wananchi ili kuweza kutunza na kuzihifadhi vyema noti hizo ili kuepusha
uchakavu unaohatarisha kushusha hali ya kiuchumi nchini.
Alisema hali ya uchumi
inashuka kutokana na gharama kubwa wanazotumia kutengenezea noti
nyingine, ili kuziingiza katika mzunguko wa fedha pindi noti
zilizokuwepo kuonekana chakavu, kutokana na utunzaji mbaya wa noti hizo.
"Changamoto kubwa
tunayukumbana nayo ni juu ya utoaji wa elimu, huku tukiwa na matumaini
elimu yetu iifikie jamii kuhusu utunzaji wa noti zetu, kwa sababu
unavyochakaza noti, inabidi tuchapishe nyingine hali inayosababisha
kutumia gharama kubwa kutengeneza noti nyingine na hapo ndipo hali ya
uchumi inapokuwa katika wasiwasi wa kushuka kulingana na gharama kubwa
inayotumika kutengeneza noti hizo," alisema Fata.
Alisema wanatumia
nafasi hiyo ya viwanja hivyo vya maonesho ya Sabasaba, kutoa elimu kwa
jamii kuhusu uhifadhi na kutunza noti hizo ili kuepuka uchakavu
unaojitokeza kwenye matumizi ya noti.
Fata alisema mbali na
kuwepo na changamoto za noti chakavu, pia uwepo wa matumizi ya noti
bandia ni moja ya changamoto zinazoikabili benki hiyo hapa nchini.
Pamoja na hayo, Fata
alisema ili kuendelea kupambana na uchakavu wa noti unaoendelea
kujitokeza BoT, inatarajia kuingiza katika matumizi sarafu ya 500 mwezi
huu ikienda sambamba na kipindi hiki cha mwaka wa fedha.
Alisema sarafu hizo za
500, zinatarajia kuanza kuingia katika matumizi mwezi huu huku
ikitarajiwa kudumu kwenye mzunguko kwa zaidi ya miaka 20,zikiwa na ubora
wake huo huo
0 comments:
Post a Comment