Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa.
Na Mwandishi Wetu
WATEJA
wanaotembelea banda la MeTL Group lililopo kwenye maonyesho ya 38 ya
Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yanayoendelea kwenye mabanda ya
SabaSaba katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa,
jijini Dar es Salaam, kesho Jumatatu wanatarajiwa kuchezeshewa droo
maalum itakayotoa zawadi mbalimbai ikiwemo pikipiki.
Katika
droo hiyo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi na atakabidhi zawadi kwa wateja mbalimbali
watakaojishindia zawadi hizo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya MeTL GROUP, Fatema
Dewji- Jaffer alieleza kuwa, droo hiyo ni maalum kwa ajili ya wateja
wote waliopata kutembelea banda hilo tokea siku ya kwanza na
kujiorodhesha majina yao. Fatema alisema MeTL
Group imeamua kutoa zawadi hizo kama shukrani na kujitangaza zaidi kwa
wateja na wananchi waliopata kutembelea na kununua bidhaa za MeTL
Group.
“Kwa
ubora wa bidhaa zetu za MeTL Group, kama inavyojulikana, ‘The
People’s Brand’, kwa droo hii wateja wetu watafurahia kwa zawadi
hizo nono” alisema Fatema.
Katika
droo hiyo, zawadi kuu ni pamoja na Pikipiki, zawadi za khanga,
vitenge, mashuka, sabuni za kuogea na kufulia, mafuta ya kupikia, unga
na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Aidha,
MeTL Group imetambulisha rasmi vinywaji vyake vipya kwenye maonyesho
hayo ya Saba Saba, ikiwemo kinywaji kinachopendwa na wengi kwenye
maonyesho hayo, MO Cola, MO Portello na MO Malt. Vingine ni MO Lemon
Mint, MO chungwa na MO Bomba (Energy drink).
0 comments:
Post a Comment