Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda.
Hayo yalisemwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akifunga sherehe za wiki ya serikali za mitaa, zilizofanyika kitaifa mkoani hapa hivi karibuni.
Alisema kimsingi wastani wa Pato la Taifa ukiligawa na idadi ya watu, inaonyesha kwa kiasi gani umaskini umepungua hapa nchini, hali ambayo inaihamasisha serikali kuongeza chachu ya maendeleo ya wananchi wake.
“Haya yote ni mafanikio ya serikali za mitaa …tumekuwa na pungufu lakini zipo jitihada za makusudi katika kuyaboresha hususan kwenye sekta mbalimbali kama kilimo, maji, elimu na nishati” alisema.
Kuhusu nishati, Pinda alisema kwa sasa idadi ya Watanzania wanaotumia umeme vijijini imeongezeka na kwamba matumizi ya gesi yatasaidia zaidi katika kulimaliza tatizo la ukosefu wa umeme kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini.
“Kwa mfano Desemba mwaka huu gesi ikishaingia Dar es Salaam kutakuwa na zaidi ya megawatts 3000, sasa mnaotaka kuwekeza tunawakaribisha sana kwa mikono miwili,” aliongeza kusema.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment