Home » » Mawaziri waijadili Burundi Dar, JK kupokea riporti

Mawaziri waijadili Burundi Dar, JK kupokea riporti

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



MAWAZIRI wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wamekutana Dar es Salaam jana ili kufanya kujadili taarifa mbalimbali zinazohusu mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Burundi.

Taarifa hizo zitawasilishwa kwa Mwenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Rais Jakaya Kikwete na Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe, alisema lengo la mkutano huo ni kujadili hali ya ukosefu wa amani ambayo imeikumba nchi hiyo.

Alisema katika mkutano huo, taarifa mbalimbali kutoka kwa vyama 45 vya kisiasa vya nchini humo zitawasilishwa ukiwemo
ujumbe wa Serikali ya Burundi ambapo Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje nchini humo atatoa taarifa kuhusu hali ya Burundi.

"Kama mjuavyo, moja kati ya nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki imekumbwa na tatizo la maandamano na ukosefu wa amani, kazi tuliyonayo leo ni kupata taarifa zote kuhusu Burundi na Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje (EAC) tutazikabidhi kwa wakuu wa nchi hizi," alisema.

Aliongeza kuwa, hadi sasa baadhi ya nchi za Afrika zimepokea wakimbizi 50,000 kutoka nchini humo ikiwemo Tanzania na Rwanda.

Mbali na mawaziri hao kuwasilisha taarifa yao, jopo la Wazee wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, nao watawasilisha taarifa zao kwenye kikao hicho.

Leo Rais Kikwete na marais wengine akiwemo Zuma, watapokea taarifa rasmi ya kikao hicho kutoka kwa mawaziri hao ambapo mkutano huo umewajumuisha pia Wajumbe kutoka COMESA, Umoja wa Afrika (AU), Umoja wa Mataifa (UN), Makamu wa
Rais wa zamani kutoka nchini Uganda, Dkt. Specioza Kazibwe.

Chanzo Gazeti la Majira

 

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa