Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku.
Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) imeandaa mkutano wa kujadili hali ya amani nchini utakaowashirikisha viongozi mbalimbali wakiwamo marais wastaafu.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Joseph Butiku, aluisema jana jijini Dar es Salaam kuwa mkutano huo ambao utafanyika kwa siku mbili kuanzia leo, pia watahudhuria viongozi wa dini, mawaziri wakuu wastaafu na viongozi wa vyama vya siasa.
Butiku aliwataja marais wastaafu watakaohudhuria mkutano huo kuwa ni Ali Hassan Mwinyi; Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
Wengine ni mawaziri wakuu wastaafu, John Malecela na Jaji Joseph Warioba wakati viongozi wa vyama vya siasa watakaokuwapo ni Katibu Mku wa Chadema, Dk Willibrod Slaa; Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahimu Lipumba na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Kwa mujibu wa Butiku, lengo la kuwashirikisha viongozi hao ni kutafakari na kujadili hali ya amani, umoja na utulivu wa nchi kwa kuzingatia kuwa viongozi hao ndio wenye jukumu na wajibu wa kusimamia amani na umoja na kuhakikisha misingi yake inaimarishwa na kudumishwa.
Alisema viongozi wanalo jukumu na wajibu wa kutambua na kuona hatua gani muhimu zinahitajika kuchukuliwa katika kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa kisiwa cha amani na mfano wa kuigwa na mataifa mengine.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment