Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kulia
mbele ni Programu Ofisa wa TGNP Mtandao, Deo Temba akiwasilisha mada
kwa washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi
Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa
habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini
Tanzania (bloggers) mara baada ya semina hiyo.
Baadhi ya maofisa kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) wakifuatilia mada anuai zinazowasilishwa.
Kushoto
mbele ni Anna Sangai na Anna Kika ambao ni maofisa programu kutoka TGNP
Mtandao wakiwasilisha mada kwa kwenye mjadala wa wachora katuni,
wasanii na waandishi wa habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa
mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers).
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi
Mkuu 2015 wakiwasilisha kazi za vikundi vyao kwenye mafunzo hayo.
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi
Mkuu 2015 wakiwasilisha kazi za vikundi vyao kwenye mafunzo hayo.
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi
Mkuu 2015 wakiwasilisha kazi za vikundi vyao kwenye mafunzo hayo.
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi
Mkuu 2015 yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa
habari pamoja na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini
Tanzania (bloggers) wakiwa katika semina hiyo.
washiriki
wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015
yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja
na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers)
mara baada ya semina hiyo.
washiriki
wa mafunzo ya kuripoti habari za wanawake katika Uchaguzi Mkuu 2015
yaliowashirikisha wachora katuni, wasanii na waandishi wa habari pamoja
na baadhi ya waendeshaji wa mitandao ya jamii nchini Tanzania (bloggers)
mara baada ya semina hiyo.
Na Joachim Mushi,
WANAHARAKATI
Ngazi ya Jamii nchini wametoa madai kuelekea Uchaguzi Mkuu huku
wakiiomba Serikali iharakishe mchakato wa uandikishaji daftari la kudumu
la wapiga kura ili vijana wengi wanaostahili waweze kuitumia haki yao
ya msingi ya kushiriki mchakato wa uchaguzi na ule wa kura ya maoni.
Madai
hayo yametolewa katika tamko lao lililotolewa na Mtandao wa Jinsia
Tanzania (TGNP Mtandao) kwenye warsha ya majadiliano kati ya waandishi
wa habari, wachora katuni na waandishi wa habari za mitandao ya jamii
iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Katika
madai hayo wanaharakati ngazi ya jamii pia wameomba elimu ya uraia na
ya mpiga kura itolewe kwa wingi ili iwafikie vijana wapate hamasa ya
kujitokeza kugombea na kupiga kura, ikiwa ni pamoja na kuvitaka vyama
vya siasa kuweka mfumo wa uwiano kwa wanawake, vijana na watu wenye
ulemavu waweze kupata nafasi sawa kama wagombea kwenye uchaguzi bila
upendeleo wala woga.
Aidha
imetaka vijana wanaojitokeza kama wagombea wawekewe mazingira rafiki
ikiwezekana wapewe ruzuku ya kuwasaidia kushindana kwenye uwanja wa
demokrasia, pamoja na kushauri Sera ya Taifa ya Vijana pamoja na Mkataba
wa Vijana wa Afrika unalitambua kundi la vijana kama rasilimali
mojawapo muhimu sana kwenye maendeleo na pia katika kulinda amani na
utulivu kwenye Bara la Afrika.
“…Hata
hivyo pamoja na kwamba vijana ni zaidi ya 60% bado mchango na thamani
ya vijana haujatumika ipasavyo kwenye demokrasia ya Tanzania, huku
thamani yao ikionekana tu nyakati za uchaguzi kwa kutumiwa kama walinzi
au wapambe wa wagombea,” imeeleza sehemu ya tamko hilo.
Limebainisha
kuwa pamoja na uanzishwaji wa Mabaraza ya Vijana kwa vyama vingi, mengi
hayana nguvu ya maamuzi kwa kuingiliwa na vyombo vya juu vya Chama,
ikiwa ni pamoja na kukumbusha kuwa mwaka 2010 ulikuwa ni mwaka ambao
vijana wengi waliingia Bungeni na wamekuwa chachu kubwa ya kuchangia na
kuibua mijadala yenye tija Bungeni.
Hata
hivyo imeeleza kuwa bado idadi ya vijana wanaojitokeza kupiga kura hasa
wasichana bado ni ndogo ukilinganisha na ile ya wanaojiandikisha na
wanaoshiriki kwenye kampeni, vijana wengi wanaojitokeza kwa kuweka nia
ya kugombea wamekumbana na kigingi cha uteuzi kwa kutokubalika ndani ya
vyama kwa mawazo mgando kwamba umri wao hauwawezeshi kufanya uchambuzi
wa masuala makubwa ya kitaifa, kadhalika changamoto ya nguvu yao ndogo
kiuchumi ajira ambayo inawafanya wasiweze kushindana kikamilifu katika
uwanja usio na usawa wa siasa.
Kwa
upande wa vyama vya siasa tamko hilo limetaka watu wenye ulemavu
waingizwe kwenye sera na mipango ya nchi kwa vitendo kwani bado ushiriki
wao kwenye masuala ya uchaguzi na uongozi uko chini.
Madai
mengine ni pamoja na Vyama vya siasa kuweka mfumo wa uwiano kuhakikisha
zinazingatia ushiriki wa watu wenye ulemavu kwenye uchaguzi kama
wagombea na wapiga kura, Serikali kuweka mazingira rafiki kwa watu wenye
ulemavu ili washiriki kikamilifu kwenye michakato yote ya maendeleo,
hii ni pamoja na uchapishaji wa sheria na kanuni kwa lugha rahisi
ikiwemo maandishi ya nukta nundu, vituo rafiki vya kampeni na kupiga
kura kwa watu wenye ulemavu.
Mengine
ni pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi, kudai ulinzi na usalama wa
maisha yao, kama raia wa taifa hili, uwepo wa mikakati ya kuelimisha
umma uondokane na mawazo potofu yanayoashiria kutishia uhai na usalama
wa kundi hili na hasa wenye ulemavu wa ngozi. Hatua kali za kisheria
zichukuliwe kwa wote watakaohusika.
“…Serikali
ihakikishe upatikanaji wa taarifa na maarifa kwa njia rahisi ikiwemo
lugha ya alama na maandishi ya nukta nundu kutoa elimu ya mpiga kura na
pia vyombo vya habari kama vile TV ziweke wakalimani hasa katika vipindi
vya taarifa ya habari na vipindi vyote vyenye mijadala ya kitaifa.
Mgombea tutakayempa kura ni Yule ambaye miongoni mwa sera zake itakua ni
kupinga ukatili wa kijinsia kwa hali zote bila woga wala upendeleo
Aidha
mengine ni pamoja na Serikali itakayoingia madarakani kuhakikisha
inaunda Tume ya Kughulikia Ukatiki wa Kijinsia kama zilivyo Tume
nyingine, kuunda mahakama maalum ya kushughulikia kesi za ukatili wa
kijinsia ngazi ya familia na kuweka mikakati halisi ya kuhakikisha
kwamba kila mwanamke ana haki ya uchumi na haki ya maisha endelevu/ajira
akiwa kijijini au mjini, mwenye ulemavu, mzee au kijana, wanawake na
wanaume wote wapate kipato kinachotosheleza kuishi maisha bora kama
binadamu.
Warsha
hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na TGNP Mtandao kwa ushirikiano na
Mfuko wa Wanawake Tanzania (TWF) imejumuisha makundi mbalimbali ya
wanahabari ikiwa ni lengo la kuwajengea uwezo kuandika masuala ya
kijinsia kwa kina.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
0 comments:
Post a Comment