Home » » SUMAYE AWANOA VIJANA

SUMAYE AWANOA VIJANA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amewataka vijana nchini kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura ili wapate fursa ya kuchagua viongozi wanaowataka, lakini pia wanaoamini watakuwa suluhisho ya kero nyingi walizonazo wananchi.

Aidha, amewataka kuwapima wagombea kwa hoja na ukomavu wao katika suala la uongozi, badala ya kuhadaika na fedha zinazotumika kununua wapiga kura, akisema `biashara’ hiyo ya kununua kura itakuja kuwaliza Watanzania.
Aliyasema hayo juzi jijini Dar es Salaam alipokuwa anazungumza na jumuiya ya wanachuo wa Chuo cha Ustawi wa Jamii.
“Vijana mna nafasi kubwa kuamua kukomesha tabia za rushwa katika uchaguzi mkuu, kwani mko wengi nchini na mna ushawishi... hivyo mkiungana na kuamua rushwa sasa basi, nchi hii itapata viongozi bora watakaoinua ustawi wa Watanzania badala ya kuwanyonya.” alisema Sumaye.
Aidha, alitumia fursa hiyo kuwataka wanachuo hao kama sehemu ya vijana waliobahatika kupata elimu nchini, kuitumia vyema fursa ya kuelimisha waliyopata ili inufaishe wengi, badala ya wao pia kugeuka wabinafsi na wenye kujinufaisha huku mamilioni ya Watanzania wakiteseka katika lindi la umasikini.
Chanzo:Habari Leo

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa