Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Kocha
Mkuu wa timu ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro, Charles Mkwasa amesema vijana wake wapo tayari kuwavaa
Nigeria Septemba 05, 2015 katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za
AFCON mwaka 2017.
Mkwasa
ambaye yupo nchini Uturuki na kikosi cha timu ya Taifa kambini kwa
mazoezi ya takriban wiki moja, amesema vijana wameonyesha mabadiliko
makubwa baada ya kupata wiki moja ya mazoezi ya pamoja.
“Mazoezi wanayofanya hapa yamewajenga
stamina, unaweza kuona wanacheza kwa nguvu muda wote, wanakaba na
kushambulia kwa pamoja, hii ni dalili nzuri ya vijana kuelekea katika
mchezo huo dhidi ya Nigeria”amesema Mkwasa.
Kocha huyo wa timu ya Taifa amesema timu
yake imefanya mazoezi katika nyanja zote ikiwemo mazoezi ya kujenga
mwili na kucheza mpira wa kasi.
Aidha Mkwasa amesema kambi hiyo imekua
na faida kubwa sana kiufundi, kufuatia kupata nafasi ya kukaa sehemu
tulivu na wachezaji kuwapa mazoezi ambayo waliyapanga katika program
hiyo ya kambi nchini Uturuki.
Taifa Stars imeendelea na mazoezi leo
asubuhi, na inatarajiwa kufanya mazoezi yake ya mwisho kesho siku ya
jumatau, kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani Tanzania kwa
maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment