Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA
Bodi
ya Ushauri, Menejimenti na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA) wanasikitika kutangaza kifo cha Mwenyekiti wa Bodi ya
TAA, Inj. Lambert W. Ndiwaita kilichoteka tarehe 20/08/2015
katika Hospitali ya Nairobi, Kenya. Marehemu anatarajiwa kuzikwa
nyumbani kwake mjini Bukoba tarehe 25/08/2015.
Mhandisi
Lambert Ndiwaita (64) ni mmoja wa wataalamu waliobobea katika masuala
ya usafiri wa anga kitaifa na kimataifa, katika kipindi cha uhai wake
ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini na
nchi nyingine duniadi.
Alianza
shughuli zinazohusiana na usafiri wa anga mwaka 19971 alipoajiriwa na
iliyokuwa Wizara ya Ujenzi kama Mhandisi Msaidizi na baadaye
alipanda hadi kufikia cheo cha Mhandisi Mkuu (Chief Engineer)
akishughulikia masuala ya baeabara na viwanja vya ndege.
Mwaka
1993 alikwenda kufanya kazi katika Idara ya Usafiri wa Anga nchini
Botswana kwa mkataba wa mwaka mmoja. Mwaka 1994 aliajiriwa na Shirika
la Kimataifa la Usafiri wa Anga International Civil Aviation
Organization (ICAO) kusimamia masuala ya viwanja vya ndege (Aerodrome
& Ground Aids) kwa eneo la Mshariki na kusini mwa Afrika, katika
ofisi za ICAO zilizopo jijini Nairobi, Kenya.
Mhandisi
Ndiwaita ni msomi aliyehitimu Shahada ya kwanza ya Uhandisi (Bsc Civil
Engineering) katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Mwaka 1978 alihitimu masomo
Shahada ya Uzamili (Msc in Civil Engineering) katika Chuo kikuu cha
Califonia, Berkley, nchini Marekani akijitikita zaidi katika masuala
uhandisi wa ujenzi wa viwanja vya ndege.
Marehemu
Lambert Ndiwaita atakumbukwa na wadau wa usafiri wa anga nchini na
duniani kwa mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta hiyo ambapo
kwa hapa nchini akiwa Mwenyekiti wa Bodi ya TAA amechangia
kufanikisha ujenzi na uboreshaji wa viwanja kadhaa vikiwemo Mwanza,
Tabora, Kigoma, Songwe,Mafia, Mpanda, Bukoba na Julius Nyerere (JNIA).
Mungu ailaze roho marehemu mahala pema peponi.
Imetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu-TAA.
24th AUGUST, 2015
0 comments:
Post a Comment