Home » » Dkt Magufuli atangaza kiama kwa wakurugenzi nchini ndani ya siku 15

Dkt Magufuli atangaza kiama kwa wakurugenzi nchini ndani ya siku 15

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 15 kuanzia leo kwa wakurugenzi wote wa taasisi za serikali kupitia upya majina ya waajiriwa wao.

Dkt Magufuli amesema lengo la kufanya hivyo ni kuondoa majina yote ya wafanyakazi ambao ni hewa ambao wanalipwa fedha kila mwezi wakati kazi hawafanyi na hawapo katika maeneo yao ya kazi.

''Mwezi uliopita tulilipa mishahara ya wafanyakazi bilioni 500 mpaka 550 tukalipa na madeni ya nje bilioni 800 ,katika malipo ya wafanyakazi wengi ni mishahara hewa na serikali inalipa''.

''Sasa kuanzia leo wakurugenzi wote wapitie majina ya wafanyakazi na ambao hawapo kazini wayaondoe majina hayo haraka iwezekanavyo na wakurugenzi ambao hawatafanya hivyo ndani ya siku 15 watafukuzwa kazi na kupelekwa mahakamani''

Aidha Rais Dkt Magufuli amewataka wakuu wa mikoa kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuwa tayari wamesaini kiapo cha kutumikia wananchi kwa uadilifu, weledi na kuzingatia sheria na taratibu za utumishi wa umma.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa