Wednesday, August 3, 2016

Kilele Maadhimisho Siku ya vijana Kitaifa kufanyika Mkoani Simiyu.

 mavi1 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Anthony Mavunde akiongea na waandishi wa Habari leo Jijijni Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani inayoadhimishwa Kitaifa tarehe 14/10/2016,Mkoani Simiyu ambapo vijana wametakiwa kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa na Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajiara na Wenye Ulemavu.
mavu2 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Anthony Mavunde akisisitiza umuhimu wa wa wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia jitihada za Serikali kuwawezesha Vijana kiuchumi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajiara na Wenye Ulemavu.
mav3 
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Anthony Mavunde na waandishi wa Habari leo Jijijni Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani itakayoadhimishwa Kitaifa tarehe 14/10/2016,Mkoani Simiyu.
(Picha na Frank Mvungi-Maelezo

Frank Mvungi-Maelezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi siku ya Kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Simiyu Oktoba 14 mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Antony Mavunde wakati wa mkutano na waandishi wa Habari.
Mhe Mavunde amebainisha kuwa Kauli mbiu ya Siku ya Vijana mwaka huu ni “Tokomeza umasikini kwa uzalishaji endelevu na matumizi yenye tija”.
Akifafanua kuhusu kauli mbiu hiyo Mhe. Mavunde amesema lengo la kauli mbiu hii ni kuzihimiza nchi wanachama wa umoja wa mataifa kushirikisha kikamilifu Vijana katika shughuli za uzalishaji na kuhakikisha kuwa panakuwepo na matumizi sahihi ya rasilimali za nchi kama vile ardhi,maji,madini na Nishati ili kufikia shabaha ya kuwa na maendeleo endelevu ifikapo 20130.
Akizungumzia maadhimisho hayo Kitaifa Mhe . Mavunde amesema kuwa vijana watapata fursa ya kushiriki shughuli mbalimbali kama makongamano,matamasha,michezo,maonnyesho ya Kazi za Vijana,Shughuli za kujitolea na maandamano ya amani.
“Tanzania tutasherekea siku ya Vijana Duniani Kitaifa kuanzia tarehe 8/10/2016 na kilele kitakuwa tarehe 14/10/2016 Mkoani Simiyu ambapo Sherehe hii itaenda sambamba na Maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Wiki ya Vijana Kitaifa na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016.” Alisisitiza Mhe. Mavunde.
Wazo la kuwa na siku ya Vijana Duniani lilitolewa katika Mkutano wa Vijana wa Kimataifa mwaka 1991 Mjini Vienna Australia kwa madhumuni ya kutafuta njia ya kuchangisha fedha za kusaidia mifuko ya Taifa ya Vijana ambapo mwaka 2000 nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania zilianza kuadhimisha siku ya Vijana Duniani kulingana na mazingira yake kwa kuzingatia kauli mbiu ambayo huandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment