Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe.Anthony Mavunde akiongea na waandishi wa Habari leo Jijijni Dar es
salaam kuhusu maadhimisho ya siku ya Vijana Duniani inayoadhimishwa
Kitaifa tarehe 14/10/2016,Mkoani Simiyu ambapo vijana wametakiwa kutumia
fursa zilizopo kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii.Kulia ni
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa na Kushoto
ni Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajiara
na Wenye Ulemavu.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe.Anthony Mavunde akisisitiza umuhimu wa wa wadau mbalimbali
kujitokeza kusaidia jitihada za Serikali kuwawezesha Vijana kiuchumi.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Vijana Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi
Vijana Ajiara na Wenye Ulemavu.
Baadhi
ya Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Anthony Mavunde na
waandishi wa Habari leo Jijijni Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya siku
ya Vijana Duniani itakayoadhimishwa Kitaifa tarehe 14/10/2016,Mkoani
Simiyu.
(Picha na Frank Mvungi-Maelezo
Frank Mvungi-Maelezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi siku
ya Kilele cha maadhimisho ya siku ya Vijana Kitaifa yatakayofanyika
Mkoani Simiyu Oktoba 14 mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini
Dar es salaam na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Antony Mavunde wakati wa mkutano na waandishi wa
Habari.
Mhe Mavunde amebainisha kuwa
Kauli mbiu ya Siku ya Vijana mwaka huu ni “Tokomeza umasikini kwa
uzalishaji endelevu na matumizi yenye tija”.
Akifafanua kuhusu kauli mbiu hiyo
Mhe. Mavunde amesema lengo la kauli mbiu hii ni kuzihimiza nchi
wanachama wa umoja wa mataifa kushirikisha kikamilifu Vijana katika
shughuli za uzalishaji na kuhakikisha kuwa panakuwepo na matumizi sahihi
ya rasilimali za nchi kama vile ardhi,maji,madini na Nishati ili
kufikia shabaha ya kuwa na maendeleo endelevu ifikapo 20130.
Akizungumzia maadhimisho hayo
Kitaifa Mhe . Mavunde amesema kuwa vijana watapata fursa ya kushiriki
shughuli mbalimbali kama makongamano,matamasha,michezo,maonnyesho ya
Kazi za Vijana,Shughuli za kujitolea na maandamano ya amani.
“Tanzania tutasherekea siku ya
Vijana Duniani Kitaifa kuanzia tarehe 8/10/2016 na kilele kitakuwa
tarehe 14/10/2016 Mkoani Simiyu ambapo Sherehe hii itaenda sambamba na
Maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius
Kambarage Nyerere, Wiki ya Vijana Kitaifa na kilele cha mbio za Mwenge
wa Uhuru mwaka 2016.” Alisisitiza Mhe. Mavunde.
Wazo la kuwa na siku ya Vijana
Duniani lilitolewa katika Mkutano wa Vijana wa Kimataifa mwaka 1991
Mjini Vienna Australia kwa madhumuni ya kutafuta njia ya kuchangisha
fedha za kusaidia mifuko ya Taifa ya Vijana ambapo mwaka 2000 nchi
wanachama wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania zilianza kuadhimisha siku
ya Vijana Duniani kulingana na mazingira yake kwa kuzingatia kauli mbiu
ambayo huandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
0 comments:
Post a Comment