Mh. Halima Mdee Mbunge wa Jimbo la Kawe, Picha na Fredy
Njeje/Blogs za Mikoa
Na Godfriend Mbuya
Mbunge wa Jimbo la
Kawe kupitia CHADEMA Halima James Mdee amesema kama Mungu akimpa uhai
mwaka 2020 katika uchaguzi Mkuu atajipima kama ametekeleza ahadi za
wananchi kama alivyoahidi ndipo atagombea kama atakuwa hajafikisha
asilimia 50 ataachia mtu mwingine.
Akizungumza katika
kipindi cha HOTMIX kinachorushwa na EATV Mdee amesema, Mwaka 2020
hatakuwa na sababu ya msingi ya kugombea kama hajaweza kufanya kitu kwa
wananchi wa jimbo lake.
“Nitaangalia kama
nimefikia asilimia 50% ya utekelezaji wa ahadi za wananchi ndipo
nitafanya hivyo ila nisipotekeleza nitapisha ili mtu mwingine mwenye
maono zaidi ya ya kwangu aweze kugombea na kuongoza jimbo hilo”-Amesema
Mdee
Aidha Mdee amesema kwa
sasa nimefanikiwa kutatua baadhi ya kero za wananchi kama maji katika
baadhi ya maeneo, na barabara nyingine zimetengewa fedha na serikali
hivyo zitajengwa na kwenye ardhi amefanikiwa kwa kushirikiana na
wananchi kutatua migogoro ya adrhi katika maeneo ya Magwepande, Bunju, na Kunduchi ambapo bado naendelea na kazi hiyo katika maeneo mengine.
Kwa upande mwingine
Mdee amesema suala la kufanya mikutano ya hadhara atafanya kulingana na
Katiba na sheria za nchi zinavyoruhusu na si vinginevyo.
0 comments:
Post a Comment