Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda
ameliagiza jeshi la polisi Jijini Dar es salaam kuhakikisha kwamba
sheria zinafuatwa na kusiwepo kitu kinaitwa UKUTA ili wananchi waendelee
na kazi zao kama kawaida.
Akizungumza na kikosi cha kutuliza ghasia katika
kambi ya Ukonga Jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa amesema kwa kuwa
askari wanafahamu sheria wasisubiri mtu yeyote kuja kuwakumbusha juu ya
jambo hilo au maelekezo mengine kwa kuwa Amiri Jeshi ambaye ni Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshaagiza kinachotakiwa ni
utekelezaji.
‘’Msisubiri maelekezo yoyote kutoka juu, asiwepo
mtu yeyote atafunga duka kwa sababu ya UKUTA nyie ni matrekta hakuna
UKUTA unaweza kusimama mbele yenu, mimi kama Mkuu wa Mkoa ninaamini
hatutakuwa na vurugu kwenye Mkoa wetu na hatuwezi kuruhusu vurugu kwa
kuwa tunajua madhara ya vurugu’’ Amesema Makonda.
Aidha kwa upande wake Kamanda wa Oparesheni Kanda Maalumu ya Dar es salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya amesema jeshi
la polisi lipo vizuri na vijana wameandaliwa vizuri na wameandaliwa
kuwa tayari siku nyingi na hakuna mtu yeyote atakayethubutu kufanya
UKUTA na watakaofanya hivyo watazimwa kabla hawajafanya chocchote.
Kamada amewaytaka wananchi
wote Jijini Dar es salaam kuto jitokeza kwenye oparesheni UKUTA kwa
kuwa maadamano hayo siyo halali na watakaojitokeza watapata matatizo
yasiyowahusu.
0 comments:
Post a Comment