Na Daudi Manongi-MAELEZO
Bodi
ya Nishati Vijijini (REB) imemteua Mhandisi Boniface Gissima
Nyamo-Hanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala
Dk.Lutengano Mwakahesya aliyestaafu mwezi Juni 2016.
Kwa
mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na Mwenyekiti wa
Bodi ya Nishati Vijijini Dk.Gideon Kaunda inaeleza kuwa uteuzi huo
umefanyika kwa mujibu wa Sheria namba 8 ya mwaka 2005 ya Nishati
Vijijini katika kikao kilichofanyika Tarehe 17 Desemba 2016.
Aidha
taarifa hiyo inaeleza kuwa kabla ya uteuzi huu Mhandisi Gissima
Nyamo-Hanga alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini
(REA).
Imeongeza
kuwa Mhandisi Gissima ana uzoefu wa miaka 20 katika Sekta ya Nishati na
pia ameshika nyadhifa mbalimbali tangu mwaka 2008 alipoajiriwa REA.
Mbali
na hayo Mhandisi huyu amehitimu Shahada ya Uhandisi katika fani ya
Umeme, Shahada ya Uzamili katika Menejimenti ya Uhandisi,Shahada ya
Uzamili ya Usimamizi wa Biashara (MBA) zote kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Stashahada ya Juu ya Sheria na Upatanishi na Usuluhishi ya Chuo
cha Ustawi wa Jamii Dar es Salaam.
Bodi
ya Wakala wa Nishati ya Umeme Vijijini (REA) inaomba sekta mbalimbali
kumpatia ushirikiano Mhandisi Boniface Gissima Nyamo-Hanga ili
kumuwezesha kutekeleza majukumu na malengo yake.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment