Waziri
wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa miundombinu ya usalama barabarani
katika shule za Msingi Mikumi na Mzimuni ikiwa ni mwendelezo wa mpango
wa uboreshaji wa usalama barababarani kwa wanafunzi wa shule za msingi
jijini Dar es Salaam ambao unaratibiwa na shirika la Amend kwa ufadhili
wa Mfuko wakampuni ya Puma Energy na Mfuko wa FIA. Wanaoshuhudia ni
pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe
Corsaletti, walimu na maofisa wa Jeshi la Polisi kikosi cha usalama
Barabarani.
Waziri
wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akikabidhi
msaada wa jaketi la usalama barabarani kwa mwanafunzi Nuru ambae ni Muhanga wa
ajali za barabarani. Nuru alilazimika kukaa hospitali kwa kipindi cha miaka
miwili akipatiwa matibabu baada ya kugongwa na gari maeneo jirani na shule
hiyo.
Waziri
wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama
akishirikiana na wanafunzi wenye ulemavu kutoka shule ya Gilman Rutihimaba kuimba
nyimbo zenye mafunzo ya usalama barabarani.
Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe Corsaletti
akizungumza kwenye hafla hiyo.
Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu,
Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy
Tanzania, Bw Philippe Corsaletti, walimu na wanafunzi
wa shule za Msingi Mikumi na Mzimuni.
Waziri
wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akiwa
kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe Corsaletti, na
maofisa wa shirika la Amend, Jeshi la
Polisi kikosi cha usalama Barabarani, walimu
wa shule za Msingi Mikumi na Mzimuni.
Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu,
Jenista Mhagama akigagua miundombinu ya usalama barabarani iliyojengwa kupitia
mpango huo. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe Corsaletti
No comments:
Post a Comment