Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI WAPEWA ANGALIZO KUHUSU SIASA

WATENDAJI WAKUU WA SERIKALI WAPEWA ANGALIZO KUHUSU SIASA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Serikali imewaagiza watendaji wake wakuu kujiepusha na siasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu mwakani, badala yake waendelee kuwa watiifu kwake na rais aliye madarakani.

Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alipokuwa akifunga mkutano wa makatibu wakuu wa wizara na makatibu tawala wa mikoa mjini hapa.

Alisema viongozi hao ambao ndiyo watendaji wakuu serikalini hawapaswi kujiingiza kwenye mihemko yakisiasa wakati wa uchaguzi mkuu mwakani kwa kuwa ni watumishi wa umma na siyo wanasiasa.

“Joto la siasa wakati wa uchaguzi linapanda sana, nawaasa msijisahau kwamba utii na uaminifu wao ni kwa Rais aliyeko madarakani na serikali yake mpaka rais mwingine atakapopatikana na kuapishwa,” alieleza Balozi Sefue.

Alisema wao kuwa watendaji wakuu wa serikali, wanawajibika kuhakikisha uchaguzi mkuu unakwisha salama,  na wawashauri wanasiasa bila kuingizwa kwenye siasa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma badala ya maelekezo ya wanasiasa.

Katika hatua nyingine, Balozi Sefue alisema kura ya maoni ya kupitisha ama kuikataa Katiba inayopendekezwa itafanyika kabla ya uchaguzi mkuu wa mwakani.

“Mchakato wa Katiba Mpya hautaahirishwa kupisha uchaguzi mkuu, utaendelea kama ambavyo sheria inaelekezwa na mkanganyiko wa tarehe ya kuanza rasmi shughuli za upigaji wa kura ya maoni anaoonekana kwenye kauli za viongozi kutokana na mambo mengi yanayotakiwa kushughulikiwa kabla ya hatua hiyo kutekelezwa,” alisema.

Alisema mpaka sasa mpango uliyopo ni kuwa wakati wowote kuanzia mwishoni mwa Aprili, shughuli hizo zinaweza kuanza na kusisitiza kuwa serikali haijaamua wala kutamka tarehe rasmi ya kufanyika kura ya maoni.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa