Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » JUST IN:TAARIFA TULIZO ZIPATA MPAKA SASA KUHUSU KIFO CHA MWIGIZAJI STEVEN KANUMBA...

JUST IN:TAARIFA TULIZO ZIPATA MPAKA SASA KUHUSU KIFO CHA MWIGIZAJI STEVEN KANUMBA...Taarifa kutoka kwa millardayo.com ambaye ameongea na  mwigizaji Dino, ni kwamba kweli mwigizaji STEVEN KANUMBA amefariki dunia na inaaminika chanzo cha kifo chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake, alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.
Polisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba muda mfupi uliopita baada ya kuwachukua waliokua wanaishi na Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya kilichotokea.
Bado watu wanazidi kuongezeka nyumbani kwa Kanumba ambapo tayari idadi kubwa ya wasanii wenzake wamefuka pamoja na watu mbalimbali, millardayo.com itaendelea kukufahamisha kinachoendelea kadri taarifa zitakavyozidi kupatikana.
Ila kumekua na taarifa nyingine ambazo hazijathibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake ambae anatajwa kuwa ni mwigizaji LULU kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.
‘Inasemekana’ Kanumba wakati akijiandaa kutoka saa sita usiku aliingia bafuni kuoga, alipotoka alimkuta Lulu akiongea na mwanaume mwingine kwenye simu ndipo alipokasirika na ugomvi kuanza.
Alipelekwa hospitali Muhimbili ambako muda mfupi baadae alifariki dunia, mwili wake bado uko katika chumba cha 

kuhifadhia maiti Muhimbili hospital.Kwa mtanzania popote pale ulipo shabiki na mpenzi wa fani ya filamu Tanzania na shabiki wa marehemu Steven Kanumba tunajua umeguswa kuwa kiasi kikubwa sana kuhusiana na msiba huu Ilikuweza kufanikisha maandalizi ya kumpumzisha marehemu Steven Kamumba toa mchango wako kwa namba zifuatazo TIGO PESA 0765111135, TIGO PESA 0713620962.  Mchango wako ni muhimu sana kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kumpumzisha marehemu Steven Kanumba,0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa