Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » UCHUNGUZI KUTOKA POLISI: Jacky Daniel" imechangia kifo cha Kanumba

UCHUNGUZI KUTOKA POLISI: Jacky Daniel" imechangia kifo cha KanumbaRPC wa Kinondoni-Charles Kenyela


POMBE
kali (Whisky) aina ya Jacky Daniel, imetajwa kama chanzo cha kifo cha
mwigizaji nyota wa filamu nchini, Steven Charles Kanumba aliyefariki
usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake, Sinza, Dar es Salaam.
wa Polisi Kinondoni, ACP Charles Kenyela amesema leo kwamba uchunguzi
wa awali unaonyesha hivyo, lakini bado wanaendelea na uchunguzi zaidi,
ili kujua zaidi.
ACP
Kenyela amesema kwamba Kanumba wamefanikiwa kumuhoji mtuhumiwa wa
kwanza katika tukio hilo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na katika maelelezo
yake amekanusha kumsukuma Kanumba.
Vyombo
vingi vya habari vilimnukuu ndugu wa Kanumba, Sethi jana akisema kwamba
Lulu alimsukuma mwigizaji mwenzake huyo katika ugomvi wao wa wivu wa
kimapenzi hadi akaanguka na kufariki dunia.
Akizungumza
kutokana na maelezo ya Lulu, Kamanda huyo alisema kwamba; ugomvi wao
ulitokana na Kanumba kutaka kumdhibiti Lulu wakati akizungumza na simu.
“Kanumba
aliamua kumfuata Lulu nje huku akifoka kwa sauti, akitaka aelezwe kwa
nini alitoka nje kupokea simu, huku akimtuhumu kuwa huenda alikuwa
akizungumza na mwanaume mwingine.
Baada
ya Lulu kuona Kanumba anamfuata, aliamua kukimbia kutoka nje ya geti,
lakini kabla hajafanikiwa kufungua geti, Kanumba  alimkamata na
kumrudishwa ndani. Kanumba akiwa amemshikilia, waliingia wote chumbani
na kufunga mlango. Sasa haijulikani nani aliyefunga mlango, ingawa
maelezo ya Lulu, anadai kuwa aliyefunga mlango ni Kanumba,”alisema
Kamanda huyo. 
Akiendelea
kumnukuu Lulu, Kamanda huyo anasema; “Baada ya Kanumba kufunga mlango,
alimuona akilegea na kujigonga kisogo chake kwenye ukuta wa chumba hicho
kabla ya kuanguka chini,”alisema.
Alisema uchunguzi wa tukio zima ukikamilika, hatua inayofuata ni kumpeleka Lulu mahakamani kama mtuhumiwa wa mauaji.
Kwa Hisani ya Father Kidevu Blog

5 comments:

Anonymous said...

Mi naona siku zake zilishafika kwakweli`sababu tukisema huyo demu alimsukuma ndiyo akaangukia kisogo na huku jamaa akiwa amelewa ni lahisi kufa.Pia ninauhakika huyo demu akuwa na dhamila ya kumuuwa Kanumba.Ni mambo ya kimapenzi tu.

Anonymous said...

Kutokana na maelezo hayo yote,bado kuna utata,eti ameanguka ,na kapiga kisogo,ni watu wangapi hulewa chakali na kuanguka,wengine huumia na wengine hawapati hata jeraha moja,ikawaje marehemu eti kapiga kisogo na kufa,inaelekea ni kapigwa na kitu kigumu au kizito na matokeo yake kufariki.Something went wrong.God don't like ugly,siri itafichuka tu.Rip kanumba,

Anonymous said...

TUIACHIE POLICE NA MAHAKAMA IFANYE KAZI YAKE KAMA KWELI LULU KAUA APATE AKI YAKE YA KISHERIA MAANA KATIKA SHERIA UKIPATIKANA NA KOSA , KUFUNGWA NI HAKI YAKE LAKINI TUKUMBUKE KWAMBA KUWA KATIKA ENEO LA TUKIO SIO KUWA WEWE UMETENDA KOSA IVYO SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE NA KUDHIBITSHA KAMA KWELI KATENDA LULU AU AMEKUFA TU.
MAKOSA YA JINAI SIO KUAKIKISHA KUWA KOSA LIMETENDEKA. CHA MSINGI NI KUAKIKISHA NI NANI KATENDA KOSA HILO. HIVYO UCHUNGUZI WA KINA UFANYIKE ISIJE IKAWA KAMA KESI YA ZOMBE AMBAYO MAHAKAMA ILITOA ANGALIZO KUWA UPELELEZI WAKE AUKUFANYIKA KWA KINA

Anonymous said...

uchunguzi wa kina ufanyike

Anonymous said...

Kwa mujibu wa BBC jana jioni, marehemu alikuwa mwimbaji wa nyimbo za Injili, na moja ya nyimbo zake ulichezwa...Walevi Mmeona??? Mungu Wetu katika Yesu Kristo adhihakiwi. Lulu aachiwe, marehemu alitengeneza mazingira ya kifo chake mwenyewe.

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa