Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WAZIRI NAGU: USHIRIKIANO UTASAIDIA KUKUZA UCHUMI

WAZIRI NAGU: USHIRIKIANO UTASAIDIA KUKUZA UCHUMI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk. Mary Nagu, amewataka Watanzania kushirikiana katika kukuza uchumi wa nchi.

Nagu alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati wakutiliana sahini makubaliano ya ushirikiano kati ya Shirikisho la Mafundi Samani Tanzania (Tawofe) na Furniture Center.

Makubaliano hayo yana lengo la kuhakikisha wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanashirikiana katika kuinua uchumi wa nchi kwa kutumia bidhaa za ndani.

Alieleza kuwa umoja huo unatakiwa kushirikiana na Jeshi la Kujenga Taifa na Magereza ambao wanatengeneza samani bora.

Shafik Bhatia, Mkurugenzi wa Furniture Center, alisema ushirikiano huo ni mwanzo mzuri katika kutangaza nchi kwa bidhaa za ndani.

Aliongeza kuwa kama wafanyabiashara wakubwa na wadogo watashirikiana anaamini Tanzania inaweza kupiga hatua katika maendeleo ya viwanda kama Japan na Singapore. 
Mwenyekiti wa AWOFE, Frederick Waibi, alisema ushirikiano huo umetokana na maazimio waliyotoa walipokutana na Waziri Nagu.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa