Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » TASAF YAIBUKA KIDEDEA KATIKA UZINGATIAJI WA TARATIBU ZA MANUNUZI (2013/14)

TASAF YAIBUKA KIDEDEA KATIKA UZINGATIAJI WA TARATIBU ZA MANUNUZI (2013/14)


Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF umekuwa Mshindi wa kwanza miongoni mwa taasisi za serikali na mashirika ya umma yanayofanya manunuzi makubwa nchini na hivyo kutunukiwa tuzo ya uzingatiaji wa taratibu na kanuni za manunuzi kwa kipindi cha mwaka 2013/2014.

TASAF imekuwa miongoni mwa taasisi zilizoshinda tuzo ya ubora wa manunuzi kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka 2013/2014 na kukabidhiwa tuzo katika hafla iliyofanyika mjini Nairobi nchini Kenya ambako Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga aliipokea tuzo kwa niaba ya taasisi hiyo ambayo kwa sasa iko katika jitihada kubwa za kulisaidia taifa kuondokana na umaskini kupitia mpango wake wa kunusuru kaya maskini PSSN.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw.Ladislaus Mwamanga  amesema licha ya taasisi yake kufanya manunuzi makubwa kutokana na uwingi wa shughuli za kutekeleza Mpango wa Kunusuru Kaya maskini, kanuni, taratibu na sheria za manunuzi ya umma zimekuwa zikizingatiwa kwa kiwango kikubwa. Bw. Mwamanga amesema kwa takribani miaka mitatu mfululizo TASAF imekuwa ikipata hati safi ya manunuzi na kuwa miongoni mwa taasisi za serikali na mashirika ya umma zinazofanya vizuri katika uzingatiaji wa sheria ya manunuzi nchini.

Zifuatazo ni picha za upokeaji wa tuzo hiyo zilizofanyika Nairobi-Kenya
 Mkurugenzi  Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (mwenye Kaunda suti) akiwa  na ngao ya ushindi wa kwanza ya uzingitiaji wa kanuni za manunuzi nchini kwa mwaka 2013/14

 Mkurugenzi  Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (kushoto) aliyeshika ngao ya ushindi  wa kwanza (kulia kwake) ni  Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA Bw. Marten Lumbanga.


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Susan Mlawi (kushoto) alikuwa miongoni  mwa wageni walioalikwa kwenye hafla ya kukabidhi  tuzo ya manunuzi kwa taasisi za Serikali na mashirika ya umma kwa nchi za Afrika Mashariki iliyofanyika mjini Nairobi, Kenya
 Baadhi ya viongozi wa taasisi zilizo shinda tuzo ya manunuzi  kwa mwaka  2013/14 kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa