Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Kiwanda cha General Tyre kuanza kazi -Mwijage.

Kiwanda cha General Tyre kuanza kazi -Mwijage.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Serikali imesema ipo mbioni kufufua kiwanda cha General Tyres ambacho kilisitisha shughuli zake za uzalishaji kwa muda mrefu baada ya kumlipa mwekezaji asilimia 26% alizokuwa anaidai serikali na sasa kiwanda ni cha serikali.

Kauli ya serikali imetolewa bungeni na waziri viwanda biashara na uwekezaji Charles Mwijage wakati akijibu swali la mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari (Chadema).

Nassari ametaka kujua kwanini serikali imekuwa na ahadi zisizotekezeleka hususani kwa kiwanda cha general tyres ambacho kilikuwa kikitoa matairi bora kuliko mengine katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.

Akijibu swali hilo waziri mwijage amesema kinachofanyika sasa ni kubadili mitambo ya kiwanda hicho kwa kuwa iliyokuwepo imechakaa na baada ya muda mfupi kiwanda hicho kitaanza kazi ili kiweze kuajiri mamia ya vijana wengi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa