Mbunge wa Jimbo la Ubungo-CHADEMA,John Mnyika
---

Viongozi wa BAWACHA Taifa,
Waheshimiwa Wabunge wa viti maalum,
Viongozi wa CHADEMA Jimbo la Ubungo,
Viongozi wa BAWACHA Jimbo la Ubungo,
Waheshimiwa Madiwani wa kata na viti maalum,
Viongozi wa BAWACHA toka kata zote za Jimbo la Ubungo.
Niungane
nanyi katika kumshukuru Mungu kwa kutupa uzima na kuendelea na kazi
katika mwaka mpya wa 2013. Kwa wale ambao hatujakutana mwezi huu wa
Januari, nitumie fursa hii kuwatakia mwaka mpya mwema wenye upendo na
uwajibikaji.
Nawashukuru kwa kunialika kuzungumza machache
kwenye Mkutano huu wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Jimbo la
Ubungo na niwapongeze waandaaji kwa kuweza kuwakutanisha pamoja viongozi
kutoka kata zote na wawakilishi wa wanachama kutoka katika matawi na
misingi na BAWACHA katika mitaa mbalimbali ya Jimbo la Ubungo.
Mwezi
Disemba 2012, CHADEMA taifa kiliutangaza 2013 kuwa ni mwaka wa ‘nguvu
ya umma’. Kufuatia tamko hilo la Kamati Kuu, viongozi mbalimbali wa CCM
walianza propaganda chafu kupitia vyombo vya habari kuwa CHADEMA
imetangaza mwaka wa ‘vurugu’.
Propaganda hizo zinalenga kutisha
umma, hususan wanawake wasiunge mkono vuguvugu la mabadiliko (M4C),
kujiunga kwenu kwa wingi katika Jimbo la Ubungo kunadhihirisha kuwa
wanawake hamko tayari kudanganywa kwa siasa chafu na mnaendelea kuiunga
mkono CHADEMA; asanteni sana.
Nawaomba
mkitoka hapa mkawaelimishe na wengine kuhusu maana halisi ya falsafa ya
CHADEMA ya “Nguvu ya Umma” (People’Power) ambayo imeelezwa katika katiba
ya chama ibara ya 3.A, kwamba wananchi ndio msingi na chimbuko la
kuundwa kwa dola ya nchi, na kuwa umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na
mwisho katika kuamua hatma ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa,
kudanganywa au kughilibiwa.
Miaka ya CCM kudanganya na kughilibu
umma imefika ukomo. Badala ya kusubiri mpaka mwaka 2015 ama kuwaachia
viongozi walio madarakani ambao wameshindwa kutimiza wajibu wao; mwaka
2013 ni wakati muafaka wa kutumia falsafa ya ‘nguvu ya umma’ kuwezesha
wananchi kuendeleza maamuzi na mawazo kuhusu rasilimali, uchumi na siasa
za nchi yetu.
Maandamano ni moja kati ya mbinu nyingi halali za
kidemokrasia za kusimamia uwajibikaji kwa “nguvu ya umma’ ; naamini
wanawake nanyi mtajadili mbinu nyingine wakati mkisubiri ratiba
itakayotolewa na chama taifa kuhusu kazi za mwaka huu wa 2013.
Nimeelezwa
kwamba katika mkutano huu mada mbalimbali zitatolewa, nitoe rai kwenu
kwamba katika kuzijadili mada hizo na masuala yatayojitokeza mzingatie
kauli mbiu ya BAWACHA kwamba ‘wanawake; chimbuko la maendeleo”.
Mrejee
pia maudhumuni ya BAWACHA yanayotajwa kwenye Mwongozo wa Baraza la
Wanawake wa CHADEMA kifungu cha 3 ya kutambua, kusimamia, kuendeleza na
kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika masuala mbalimbali yanayohusu
mustakabali wa chama na wa taifa kwa ujumla.
Kwa kuwa mwaka 2013
ni kipindi cha kukamilisha uchaguzi wa ndani ya chama na kuendelea na
maandalizi ya chaguzi za vijiji, vitongoji na mitaa za mwaka 2014;
mtumie pia nafasi hii kuhamasishana kugombea uongozi katika chaguzi za
ndani ya chama na chaguzi za kiserikali.
Pamoja na ajenda
zingine mlizojipangia katika mkutano wenu, napendekeza pia muingize
ajenda ya “Ukuzaji wa Ajira” hususan kwa wanawake na vijana.
Zingatieni
kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 3.B, CHADEMA ni chama cha mrengo wa kati
ambacho pamoja na mambo mengine kinaamini katika kukuza na kuimarisha
uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali za nchi yetu bila kuathiri uhuru
wa taifa na kuhakikisha umma kwa ujumla unanufaika na rasilimali hizo.
CHADEMA
inaamini kumiliki rasilimali na mali miongoni mwa wananchi kunawapa
uhuru zaidi hivyo kwa itikadi hiyo ya mrengo wa kati tunataka kujenga
chama na tukishika uongozi wa nchi; tutajenga taifa lenye kutoa fursa,
ambapo kila mtu bila kujali asili na hali yake anaweza kutimiza na
kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake.
Nchi yetu inakabiliwa na
matatizo makubwa ya ukosefu wa ajira hususan kwa wanawake na vijana; CCM
na Serikali yake wanaelekea kutotambua uzito wa matatizo hayo, ndio
maana Waziri wa Kazi na Ajira Gaudencia Kabaka tarehe 21 Machi 2012
aliitaja hali hiyo kama ‘changamoto’ tu na kutoa ufafanuzi usiokidhi
haja.
Mwezi Novemba 2012 wakati wabunge wengine tukiwa bungeni
Dodoma tukitekeleza kazi ya kuwawakilisha wananchi, Waziri Kabaka
alikuja jimboni Ubungo kwenye mahafali ya shule binafsi inayomilikiwa na
mbunge mwenzake wa CCM na kutoa kauli mbalimbali kuhusu mimi.
Kiu
ya wazazi na wanafunzi siku hiyo ilikuwa kumsikia akizungumzia kuhusu
ukuzaji wa ajira kwa vijana ikiwemo wahitimu, badala yake katika suala
hilo linalohusu Wizara yake Waziri akatoa majibu ya ujumla tu ya
kuwataka vijana kujiajiri bila kueleza mazingira ambayo serikali
imeyaweka ya kuwezesha ukuzaji na upatikanaji wa fursa za ajira nchini.
Nawashukuru
Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Jimbo la Ubungo mlimjibu kwa
kumweleza ukweli kuhusu masuala mengine ya maendeleo; wakati nikiwa
naendelea na kazi ya kuwawakilisha wananchi wote wa Jimbo la Ubungo
bungeni.
Mwezi huu wa Januari 2013 viongozi wa CCM makao makuu,
mkoa na wilaya wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wao Mwigulu Nchemba
walikuja kwa mara nyingine tena jimboni Ubungo kama ilivyokuwa 2012 na
kuendeleza propaganda. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwamba ili nchi
iendelee inahitaji siasa, lakini siasa safi.
CCM iliyoshindwa
kuwezesha maendeleo ya nchi, sasa imehamia kwenye siasa chafu, mfano hai
ni Nchemba na wenzake walivyodanganya wananchi katika mkutano wa
hadhara Manzese tarehe 14 Januari 2012 kuwa Katibu Mwenezi wa Kata hii
ya Saranga amehamia chama hicho, wakati katibu mwenezi wetu tunaye mpaka
leo.
Proganda chafu hizo zimesambaa katika CCM mpaka kwenye
taasisi zake na sasa zimefikia kwa kiwango ambacho hata viongozi
wanawake wa CCM nao wanajiingiza katika siasa chafu za kusema uongo.
Siku
chache baada ya mkutano huo wa Manzese, Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT)
nao ukafanya ziara katika katika kata hii ya Saranga na kuendeleza
uzushi huo pamoja na kuanza kuwapotosha wanawake kwamba CCM sasa
inaanzisha mikopo isiyo na riba kwa wanawake watakaojiunga na chama
hicho.
Siasa hizo chafu za uzushi zimefanyika mbele ya Katibu wa
UWT Taifa, Amina Makilagi mwaka huu wa 2013; na ni mwendelezo wa
propaganda zingine ambazo ziliwahi kutolewa mbele ya Mwenyekiti wake
Sophia Simba alipokuja jimbo la Ubungo miaka iliyopita.
Kwa kuwa
mwishoni mwa mwaka 2012 nilifanya mikutano katika kata zote za Jimbo la
Ubungo kwenye mitaa mbalimbali, sikuona ulazima wa kujibu uongo na
uzushi kwa wananchi wenye kuulewa ukweli na wanaotarajia vyama vya siasa
vifanye siasa safi za maendeleo ya nchi.
Nashukuru viongozi wa
chama na BAWACHA kata ya Saranga kwa kuamua kufanya mkutano wa hadhara
jana tarehe 19 Januari 2013 kwa kushirikiana na viongozi wa Jimbo na
kuendeleza vuguvugu la mabadiliko na kusimamia siasa safi.
Nilitarajia
Mawaziri wa Serikali kama Kabaka na Sophia Simba wanapokuja kukutana na
wananchi badala ya kufanya propaganda watumie nafasi hiyo kuwaeleza
wananchi ahadi za toka mwaka 2005 zilizotolewa na Rais Jakaya Kikwete ya
kwamba “wanawake watawezeshwa” na ‘vijana watapata ajira”.
Mwaka
huu wa 2013 nitaendeleza kutoka kazi nilizofanya kwa mwaka 2011 na 2012
nikiweka mkazo pia katika kutimiza wajibu wa kuisimamia Serikali
bungeni ieleze hatua zilizofikiwa katika kutekeleza ahadi hizo.
Kwa
upande wenu BAWACHA mtakapojadiliana kuhusu ajenda ya ‘ukuzaji wa
ajira’ katika mkutano huu, pamoja na kazi mtakazojipangia ikiwa ni
sehemu yakutekeleza dhumuni la kubuni mafunzo ya wanawake kuhusu masuala
ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ili kukabiliana na changamoto
mbalimbali; mpange pia mikakati ya kukabiliana na propaganda za UWT.
Muwaeleze
wazi wanawake wenzenu Gaudencia Kabaka, Sophia Simba na Amina Makilagi
ambao wote ni wabunge wenzangu badala ya kufanya propaganda kwamba CCM
itatoa mikopo isiyokuwa na riba au ya riba ndogo kwa wanawake waunge
mkono michango tunayotoa bungeni ya kutaka kutungwa kwa sheria ya
usimamizi na udhibiti wa mikopo midogo midogo na taasisi ndogo za fedha,
kuepushawanawake kunyonywa na wengine kuongezewa umaskini.
Aidha,
muitake Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Benki kuu iweke mifumo ya
dhamana ambavyo itawezesha riba kupungua katika mabenki na taasisi
zingine za fedha na kujengea uwezo wazalishaji na wafanyabiashara wadogo
ikiwemo wanawake na vijana kuweza kukopesheka kwa urahisi.
Mwaka
2013 umetangazwa kuwa ni mwaka wa “Nguvu ya Umma” pamoja na kutumia
falsafa hii katika ushiriki wenu kwenye kuboresha mchakato wa katiba
mpya na kutaka hatua za serikali dhidi ya kuongezeka kwa mauaji ya raia
ikiwemo yenye mwelekeo wa kisiasa;
Ni wakati pia wa wanawake na
vijana kuunganisha nguvu kutaka uwajibikaji wa Serikali kutekeleza
Mpango uliokwama miaka mingi wa Serikali kupitia Halmashauri za Wilaya
kote nchini kutakiwa kutenga asilimia 10 ya Mapato yake ya Ndani kwa
ajili ya mikopo ya masharti nafuu kwa wanawake na vijana kwa ajiri ya
kujiajiri na kuchangia katika kuinua uchumi wa nchi na kuboresha maisha
ya wananchi.
Hatua hii iende sambamba na kuongeza mtaji kwa
Benki ya Wanawake (TWB) kuiwezesha kufikia wanawake wengi zaidi ikiwemo
wa mitaani na kuanzisha Benki ya Vijana (TYB).
BAWACHA mtumie
kila nafasi kuwashauri wote mtakaokutana nao walio katika sekta ya umma,
sekta binafsi na sekta ya kiraia kwamba kuongezeka kwa mfumuko wa bei
na gharama za maisha kukichanganyika na ukosefu wa ajira ni hatari kwa
uchumi na usalama.
Hivyo, badala ya vyombo vya ulinzi na usalama
kutumia nguvu nyingi dhidi ya CHADEMA na M4C, Serikali na CCM kujikita
katika propaganda chafu na mikakati ya hujuma; nguvu za sekta zote
muhimu nchini zielekezwe katika kupambana na ufisadi, kutumia vizuri
rasilimali za taifa na kuchangia katika ‘ukuzaji wa ajira’.
Wanawake; Chimbuko la Maendeleo. Nawatakia mafanikio katika mkutano na asanteni kwa kunisikiliza

0 comments:
Post a Comment