Home » » HATARI SANA : JE DAWASCO MNAYAONA HAYA?

HATARI SANA : JE DAWASCO MNAYAONA HAYA?


Katika pitapita zetu leo mtaani Jijini Dar es salaam tumekutana na tukio ambalo kwa ukweli limetushtusha na kutuletea maswali mengi bila kupata majibu....
 Ni Baada ya Mamlaka husika Kupitisha Bomba za maji safi ndani ya Mtalo ambao unapitisha maji machafu...
Na kama haitoshi bomba hizo za maji Masafi zimepasuka na zinavuja maji kwa wingi huku maji machafu yakiwa yanapita katika eneo hilo na kuhatarisha afya za watumiaji wa maji hayo.

 Hivi ndivyo inavyo onekana ikiwa Bomba hizi za maji safi zimejichanganya na matakataka , katika kiungio kinacho onekana hapo , kwanza kimeunganishwa vibaya pili kinatoa maji na tatu kuna bomba zimetoboka hapo...

 Huu ndio muundombinu ambao kiafya haujakaa sawa sawa kwa sababu maji haya yanatumiwa na mwanadam .
 Hapa maji yamepungua sana lakini mvua zinapoanza kunyesha  husababisha usumbufu mkubwa na maji taka kuchanganyikana na maji safi na mwisho kumfikia mtumiaji, hata kama yataingia kwa kiasi kidogo lakini bado yaweza kuathiri afya ya mtumiaji

 Eneo hilo ndani ya Mtalo huo kuna Bomba limepasuka na kusababisha maji kumwagika hovyo  huku uchafu ukiwa unapita katika sehemu hiyo.
Huu ndio Muundombinu.

Hii ni Sinto fahamu ....   Mamlaka husika zifike eneo husika na kushuhudia
Picha zote na Dar es salaam yetu Blog

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa