Aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai (DCI) Robert Manumba
--
DAR ES SALAAM NOVEMBER 11, 2013.
Jeshi
la Polisi nchini linapenda kuutaarifu umma kwamba aliyekuwa Mkurugenzi
wa Upelelezi wa makosa ya jinai (DCI) Robert Manumba amefikia umri wa
kustaafu kisheria ambao ni miaka sitini(60) katika utendani wake wa
kazi.
Aidha,
katika utumishi wake ndani ya Jeshi la Polisi amefanya kazi katika
nyadhifa mbalimbali zikiwemo Chumba cha kupokea mashtaka kuanzia mwaka
(1976 – 1977), mwendesha mashtaka wilaya ya Kibondo na Kasulu mkoani
Kigoma, 1977 – 1984), Mkufunzi katika chuo cha polisi Dar es salaam,
(1984 – 1987), Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Magomeni na Kinondoni na
Naibu Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Dar es salaam (1987 – 1993),Pia,amewahi kuwa Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Arusha, ( 1993 – 1995), Mkufunzi
mkuu wa Chuo Cha Polisi Moshi ( 1995 – 1996), Mkuu wa kitengo cha Fraud
makao makuu ya upelelezi, (1996 – 1997), Mkuu wa kitengo cha usalama wa
nchi, intelijensia na madawa ya kulevya makao makuu ya upelelezi (1997 –
2001) na kuwa msaidizi wa mkurugenzi wa upelelezi wa
makosa ya jinai nchini (2001 – 2006).
Kuanzia mwaka 2006 hadi anastaafu,
alikua Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai nchini.
Aidha,
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Said Mwema, amemshukuru na
kumpongeza (DCI) Manumba anayestaafu kwa kulitumikia taifa katika
nyadhifa mbalimbali ndani ya Jeshi la Polisi kwa weledi na uwaminifu
mkubwa wakati wote alipokuwa mtumishi ndani ya Jeshi la Polisi.
Pia,
amemtaka kuendelea kuwa msaada kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa
ushirikiano wa namna yoyote ile unaoweza kusaidia kupunguza uhalifu hapa
nchini kwasababu suala la usalama ni taaluma kama zilivyo taaluma
zingine, na taaluma hiyo wanayo watu wachache.
Hata
hivyo, wakati tataratibu wa uteuzi wa mkurugenzi wa upulelezi
ukiendelea, mkuu wa ufuatiliaji na tathimini CID makao makuu,
kamishina Isaya Mungulu, atakua akikaimu nafasi hiyo.
Imetolewa na:-
Advera Senso – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
0 comments:
Post a Comment