Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco)
Washtakiwa wengine ni aliyekuwa Afisa Ugavi wa Tanesco, Hanin Mahambo, Mkurugenzi wa Fedha Lusekeo Kasanga, Mwanasheria Godson Ezekiel na Mkandarasi Martin Abraham.
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Isidori Kyando, alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa, kwamba washtakiwa walitenda makosa hayo katika tarehe tofauti mwaka 2011.
Kyando alidai kuwa shitaka la kwanza ni la matumizi mabaya ya Madaraka kuwa Desemba 2011, katika ofisi za Tanesco Ubungo, jijini Dar es Salaam washtakiwa kwa pamoja walitumia madaraka yao vibaya kwa kufanikisha malipo kwa msambazaji M/S Young Dong Electronic Co Ltd bila kuhakikisha kwamba mkandarasi anafika katika kituo cha mwisho.
Ilidaiwa kuwa washtakiwa walifanya kosa hilo kinyume na kifungu namba 35 (21) cha sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2004 na kusababisha Martin Abraham kupata faida kutokana na ukandarasi huo.
Shitaka la pili ni la kuisababishia serikali hasara linalowakabili Semtutu, Mahombo, Kasanga na Ezekiel ambao wanadaiwa kwamba kati ya Januari hadi Desemba 2011 katika ofisi za Tanesco Ubungo waliisababishia serikali hasara ya Sh. 275,040,000 kutokana na matumizi yao mabaya ya madaraka.
Washtakiwa wote walikana kutenda kosa hilo huku upande wa mashtaka ukidai kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuomba tarehe nyingine ya kuwasomea washtakiwa hao maelezo ya awali.
SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment