Home » » WAZIRI NYALANDU AKUTANA NA TAASISI MBALIMBALI ZINAZOJIHUSISHA NA UHIFADHI WANYAMAPORI JIJINI NEW YORK – MAREKANI

WAZIRI NYALANDU AKUTANA NA TAASISI MBALIMBALI ZINAZOJIHUSISHA NA UHIFADHI WANYAMAPORI JIJINI NEW YORK – MAREKANI


 Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu  akiagana na Bw. Dave Stewart kutoka Taasisi ya Vulcan inayojihusisha na masuala ya kuidadi tembo katika nchi 18 barani Afrika ikiwemo Tanzania mara baada ya kumaliza mazungumzo nao  jana jijini New York nchini Marekani.



Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu  (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa Taasisi ya inaundwa na Wanajeshi Wastaafu wa jeshi la Marekani walioanzisha umoja wao ujulikanao kama (VETPAW)kwa ajili ya kusaidia Uhifadhi wa Wanyamapori barani Afrika mara baada ya kumaliza mazungumzo baina yao jana jijini New York, Marekani.  Kushoto ni Balozi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi.



Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu  akizungumza na Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi  mara baada ya kukamilika kwa kikao jana baina ya Waziri Nyalandu na ujumbe wake pamoja na taasisi mbalimbali za uhifadhi jijini New York, Marekani. Kati ni Katibu wa Waziri Bw. Imani Nkuwi.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa