Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Jakaya Kikwete anatarajia kufungua mkutano wa
Kanda ya Afrika kuhusu Mpango wa Uendeshaji wa
Shughuli za Serikali kwa uwazi (OGP).
Kwa mujibu wa taarifa
kutoka Ikulu inaeleza kuwa mkutano huo wenye kauli mbiu isemayo “Kuimarisha
Utawala Bora Unaozingatia Uwajibikaji na Uwazi” utafanyika Mei 20 hadi 21, 2015
katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Aidha, imeeleza kuwa dhumuni
la mkutano huo ni kuleta ufanisi katika
utekelezaji wa masuala mbalimbali ya uwajibikaji na utawala wa Serikali ili
kutoa mrejesho kwa wananchi pamoja na uwazi kuhusu masuala ya ardhi.
“Kupata uzoefu wa
utekelezaji wa OGP kutoka nchi wanachama katika bara la Afrika nan je ya Afrika
kama vile taarifa za uwazi zinazoimarisha uwajibikaji” iliongeza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ilisema kuwa mkutano huo ni wa kwanza kufanyika nchini
Tanzania na ni wa pili kwa Kanda ya Afrika ambapo kwa mara ya kwanza ulifanyika nchini Mombasa nchini Kenya mwaka
2013.
Mkutano huo unatarajiwa
kuwa na washiriki 200 kutoka Serikalini, Asasi za kirai, Washirika wa Maendeleo
wakiwemo Mawaziri kutoka ndani na nje ya nchi, Makatibu Wakuu, Wakuu wa baadhi
ya Taasisi za Serikali, wawakilishi kutoka Nchi wanachana wa OGP kutoka bara la
Afrika.
Washiriki wengine ni
kutoka nchi za Botswana, Zambia, Uganda, Marekani, Zimbabwe pamoja na washirika
wa Maendeleo kutoka Benki ya Dunia, UNDP, UNICEF, UNESCO, MCC, USAID, DFID na
JICA.
0 comments:
Post a Comment