Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameyataka makampuni yanayojihusisha na mafuta na gesi nchini, kuhakikisha yanatimiza mahitaji ya Soko la Ndani na ukanda wa Afrika Mashariki kabla ya kufikia Soko la Nje.
Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Utafiti na ufunguzi wa kozi ya Shahada ya Uzamili ya Mafuta na Gesi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Katika hotuba iliyosomwa na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene alisema Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki bado una mahitaji makubwa ya rasilimali ya gesi hususani katika viwanda na nyanja zote.
“Malengo ya serikali ni kuona kuwa rasilimali hizi inakuwa kichocheo cha kukuza uchumi na maendeleo ya taifa kwa ujumla,” alisema.
Kuhusu uanzishwaji wa kozi ya uzamili Katika masuala ya gesi na mafuta, Pinda alisema juhudi zinazofanywa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, zitaisaidia nchi kulifikia lengo la Kuwa na wataalamu wa mafuta na gesi wa ndani kwa asilimia 100 Kabla ya kuanza uzalishaji wa nishati hiyo miaka Saba ijayo.
Kuhusiana na utunzaji wa mazingira, Pinda aliyataka makampuni ya mafuta na gesi kufuata sheria za kimataifa za kuhifadhi mazingira, jambo litakalofanya upatikanaji wa mafuta na gesi nchini Kuwa baraka na si laana.
Akizungumzia wiki ya utafiti, Pinda aliupongeza uongozi wa chuo hicho na kueleza kuwa serikali ilikuja na sera ya utafiti na maendeleo ya mwaka 2010 kwa kutambua umuhimu ya tafiti katika kuleta maendeleo ya uchumi.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala alisema chuo chake kwa sasa kinaendesha kozi tatu za shahada ya kwanza ya uhandisi Katika gesi na mafuta, jiolojia ya gesi na mafuta, na kemia ya mafuta na gesi na kuwa sasa wamekuja na kozi ya uzamili ya jiolojia ya mafuta na gesi lengo likiwa ni kupunguza uhaba wa wataalamu nchini.
Akizungumzia ubora wa wahitimu, Mukandala alisema kwa sasa wamekuwa wakitoa mafunzo hayo kwa wanafunzi wa chache katika na miundombinu iliyopo ili kutoa wahitimu bora na kuwa lengo la ni kufikia kutoa kazi ya uzamili katika sekta ya gesi na mafuta.
Kuhusu wiki ya utafiti, Mukandala alisema inahusisha maonesho ya tafiti mbalimbali. zilizofanywa na watafiti na wahadhiri waliopo katika vyuo vishiriki, shule kuu na taasisi zote zilizo chini ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Chanzo:Habari Leo
0 comments:
Post a Comment