Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Donan Mmbando (katikati) akipokea msaada
wa dawa za kuthibiti maambukizi ya kipindupindu kutoka kwa mwakilishi wa
shirika la Afya Duniani (WHO) Dr. Rufaro Chatora(kulia). Kushoto ni Mganga Mkuu
kutoka Wizara hiyo Dkt. Margaret Mhando.
Picha na Ally
Daud
Na Ally daud-Maelezo
Wizara ya Afya
na Ustawi wa jamii imepokea msaada wa
dawa za kukabiliana na mlipuko wa
ugonjwa wa kipindupindu nchini kutoka Shirika la Afya Duniani zenye thamani ya
shilingi milioni 42.2.
Msaada huo
umepokelewa leo jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii Nchini Dkt. Donan Mmbando.
Akizungumza mada
baada ya kupata msaada huo amesema dawa hizo ambazo ni katoni 1000 za water
guard, lita 100 za Cresol Saponated zitasaidia kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.
Naye mwakilishi
wa Shirika la Afya Duniani(WHO)
nchini Tanzania Dkt.. Rufaro Chatora amesema kuwa ni wajibu wao kusaidia
kupamabana na maambukizi ya ugonjwa huo ili kuhakikisha unatokomea nchini.
Ameongeza kuwa
ni jukumu la wananchi la kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo kwa kudhibiti
hali ya usafi kuanzia mwili , chakula na mazingira yanayowazunguka kwa ujumla.
Dkt. Chatora
amesema kuwa ni vema wananchi wakapigwa marufuku kuuza vyakula sehemu za kampeni ili
kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.
Aidha ,
Mwakilishi huyo wa WHO amesema kuwa Shirika lake litatoa msaada wa shilingi milioni
159.8 kwa ajili ya kusaidia kampeni ya kuzuia ugonjwa wa KipindupinduNchini .
0 comments:
Post a Comment