Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
21/03/2016
Dar es Salaam.
Uongozi
wa kampuni ya Kikundi cha Waadhirika wa Maendeleo (KICHAWA)
unaojishughulisha na usafirishaji wa mizigo wamezindua mwongozo wa mfumo shirikishi wa uratibu wa Bodaboda na Bajaji nchini.
Akizindua
mfumo huo leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Bw.
Mussa Chengulla na kusema kuwa lengo ni kupambana na kupata suluhiso la
kudumu katika sekta ya usafirishaji wa Bodaboda na Bajaji juu ya
changamoto za kisheria, kiusalama na kimazingira.
Chengulla
amesema kuwa sababu zilizopelekea kuanzishwa kwa mfumo huo ni matokeo
makubwa ya changamoto zilizojitokeza katika jamii juu ya wizi wa
pikipiki, wizi wa kutumia pikipiki, uvunjifu wa sheria za usalama
barabarani, kanuni za usafirishaji, matumizi ya kujichukulia sheria
mkononi, uegeshaji holela wa bodaboda na bajaji na ukamataji usio
salama.
“Uwanzishwaji wa mfumo huu shirikishi ni kukabiliana na changamoto zitokanazo katika sekta ya usafirishaji
na kutatua kero hatarishi zinazoikabili jamii ili kufika malengo ya
kuiondoa ajira ya bodaboda na bajaji katika orodha ya ajira hatarishi,
kero na janga la Taifa na kuifanya kuwa ajira tegemezi, endelevu na
salama kwa usalama wa raia na mali zao” aliongeza Bw. Chengulla.
Mbali
na hayo Bw. Chengulla amesema kuwa watakaonufaika na mfumo shirikishi
ni TAMISEMI Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya kwa kutambua idadi kamili
ya wanaoendelea kujiajiri na kuajiriwa kupitia sekta ya usafirishaji
abiria.
Pia
wengine watakaonufaika na mfumo huo shirikishi ni SUMATRA, Mamlaka ya
Mapato Nchini (TRA), Jeshi la Polisi na Usalama ya Raia na kitengo cha
usalama barabarani, wamiliki na madereva wa bodaboda na bajaji kulingana
na kazi za sekta husika.
0 comments:
Post a Comment