Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Bodi
ya Usajili ya Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) imewapiga marufuku
wanaofanya kazi za Mipangomiji bila kusajiliwa ili kuondoa usumbufu na
kupunguza udanganyifu kwa wananchi wanaohitaji huduma hiyo.
Onyo
hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Msajili wa Bodi hiyo,
Helena Mtutwa katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari kuhusu
majukumu ya Bodi hiyo.
“Kwa
mujibu wa kifungu cha 23(4) cha Sheria ya Usajili wa Wataalam wa
Mipangomiji ya 2007 inasema kuwa ,ni kosa la jinai kufanya kazi hizi
bila kusajiliwa kwa hiyo, nawashauri wafanyao shughuli hizo kuacha mara
moja”, alisema Mtutwa.
Mtutwa
amewataka wananchi wenye sifa zinazowawezesha kusajiliwa na TPRB wafike
katika ofisi zao kwa ajili ya kusajiliwa ili kuepusha usumbufu
utakaojitokeza kwao na kwa Bodi hiyo.
Aidha,
Msajili huyo amesisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi ya mwananchi yeyote atakayebainika kukiuka agizo hilo.
Bodi ya
Usajili ya Wataalam wa Mipangomiji ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa
chini ya Sheria namba 7 ya mwaka 2007 ambapo moja ya majukumu yake ni
kusajili wataalam wa Mipangomiji na kusimamia maadili.
0 comments:
Post a Comment