Na. Lilian Lundo - MAELEZO
Idadi
ya wagonjwa wa upasuaji katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya
Fahamu (MOI) imeongezeka kutoka wagonjwa 20 mpaka wagonjwa 40 kwa siku.
Meneja
Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa taasisi hiyo Jumaa Almas ameyasema hayo
leo, jijini Dar es Salaam wakati akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa
habari juu ya tuhuma zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa
taasisi hiyo inabana matumizi na kusababisha msongamano wa wagonjwa
taasisi hiyo.
Amesema
asilimia 80% ya wagonjwa walio katika taasisi hiyo wanahitaji upasuaji
wa dharura jambo ambalo limeilazimu taasisi hiyo kufungua wodi nyingine
ya upasuaji ili wagonjwa wote wanaohitaji huduma ya upasuaji wa dharura
waweze kufanyiwa ili kuokoa maisha yao.
“Msongamano
wa wagonjwa MOI hausababishwi na kubana matumizi bali ni kutokana na
kuongezeka kwa wagonjwa kutoka wagonjwa 20 mpaka wagonjwa 40 kwa siku
ambapo kumesababishwa na ongezeko kubwa la ajali hasa za pikipiki katika
jiji la Dar es Salaam,” amesema Almas.
Amefafanua
kuwa wagonjwa wa upasuaji wa kichwa na ubongo hulazimika kusubiri kwa
muda kutokana pindi wanapopelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi
mara baada ya upusuaji na kuongeza kuwa vyumba vya wagonjwa mahututi ni
vichache ikilinganishwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wanaohitaji
upasuaji huduma hiyo.
Amesema
Taasisi hiyo inategemea kuongeza vyumba vingine zaidi kwa ajili ya
wagonjwa mahututi ili kukidhi idadi ya wagonjwa ambao wamekuwa
wakiongezeka kila siku
Akifafanua
kuhusu usitishwaji wa kambi za upasuaji (surgical camps) zilizokuwa
zikifanyika siku za mapumziko amesema kuwa kambi hizo zimesitishwa kwa
muda mrefu kufuatia uamuzi wa Bodi ya wadhamini ya MOI baada ya bajeti
ya kuendesha kambi hizo kuwa kubwa ikilinganisha na mapato ambayo
taasisi imekuwa ikiyapata ambayo yamekuwa yakiigharimu Taasisi hiyo kiasi cha shilingi milioni 5 mpaka 7 kwa wiki.
Pia amekanusha suala la uuzwaji wa viungo pandikizi katika Taasisi hiyo na kusisitiza kuwa
sio la kweli bali Taasisi imekuwa ikipata msaada wa vipandikizi hivyo
kutoka Taasisi ya Sign Group International ya Marekani kwa miaka mitano
sasa na wagonjwa wamekuwa wakichangia gharama za upasuaji, dawa na
huduma nyingine.
Amesisitiza
kuwa Uongozi MOI unawahakikishia watanzania kwamba huduma taasisi hiyo
zinaendelea kama kawaida na yoyoye mwenye malalamiko juu ya huduma ya
MOI afike ofisi ya Uhusiano na Ustawi wa Jamii na malalamiko yake
yatashughulikiwa.
0 comments:
Post a Comment