Waziri wa Afya
,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
akiongea mbele ya Viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini(TFDA) hawapo pichani wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya mamlaka hiyo leo jijini Dar es salaam.
|
Waziri wa Afya
,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa
kwanza kulia akimkabidhi nyenzo za kazi Mwenyekiti mpya wa Bodi ya
Ushauri TFDA Balozi Dkt. Ben Moses kushoto wakati wa Uzinduzi wa hiyo
leo jijini Dar es salaam
|
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini(TFDA) Bw. Hiiti Sillo wa pili kushoto akifafanua jambo kwa Waziri wa Afya
,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa
kwanza kulia wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya mamlaka hiyo leo
jijini Dar es salaam.
|
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akipata maelekezo kutoka kwa wataalamu wa maabara za Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA )wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya ushauri ya mamlaka hiyo leo jijini Dar es salaam
|
Waziri wa Afya
,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
katikati akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Ushauri TFDA wakati wa
Uzinduzi wa hiyo leo jijini Dar es salaam.
Habari/Picha Na Ally Daud
Serikali
imetenga milioni 900 ili kuzalisha dawa za binadamu katika viwanda vya
ndani ili kufanya asilimia 80 ya dawa zinazoagizwa nje zipatikane
nchini.
Akizungumza
hayo wakati wa Uzinduzi wa Bodi mpya ya ushauri kutoka Mamlaka ya
Chakula na dawa nchini (TFDA), Waziri wa Afya Waziri wa Afya
,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema
kuwa Serikali imetenga fedha hizo kuhakikisha viwanda vya ndani
vinatengeneza dawa hapa nchini na kupiga hatua katika uchumi wa viwanda.
“Serikali
kupitia wizara yangu tumetenga milioni 900 ili kuzalisha dawa za
binadamu katika viwanda vya ndani ili kufika uchumi wa kati kwa kutumia
viwanda”.alisema Mhe. Ummy.
Aidha
Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA kwa kushirikiana na Serikali wanapaswa
kuhakikisha viwanda vya ndani vinatengeneza dawa zenye ubora kwa
matumizi ya binadamu ili kupunguza magonjwa yanayotokana na sumu za
kemikali zitokananzo na dawa hizo.
Mhe.
Ummy ameongeza kuwa TFDA inatakiwa ishirikiane na Taasisi ya viwango
nchini (TBS) ili kuzuia na kupiga marufuku bidhaa zisizokizi viwango na
ubora unaopaswa kutumiwa na Watanzania.
Aidha
Waziri Ummy amesema kuwa TFDA inatakiwa kutoa elimu ya kutosha kwa umma
ili kuwawezesha watanzania kuepuka kutumia bidhaa zisizo na ubora kwa
matumizi ya binadamu .
Mbali
na hayo Mhe. Ummy amesema kuwa TFDA inatakiwa ikusanye mapato kwa wingi
zaidi ili kuendana na kasi ya Rais Magufuli na kupiga hatua kiuchumi
ili isaidie wananchi katika shughuli za maendeleo.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri TFDA Balozi Dkt.Ben Moses
amesema kuwa wamepokea maagizo yote yaliyotolewa na Mhe. Waziri na
watayafanyia kazi kwa haraka na ufanisi ili kuendana na kasi ya “HAPA
KAZI TU”.
“Tumepokea
maagizo ya Mhe. Waziri na nataka kumuhakikishia kwamba tutaendelea na
kasi yetu ili kuifikisha nchi yetu kwenye kilele cha maendeleo na Afya
bora” alisisitiza Dkt. Moses.
|
0 comments:
Post a Comment