Na Godfriend Mbuya
Naibu Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson Mwansasu amesema
hakuna Mbunge ambaye ana hadhi ya juu kuliko mwingine katika Bunge ,
balli katiba inawatambua wabunge wote wapo sawa.
Akizungumza katika mahojiano maalumu katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha ITV, Naibu Spika amesema makundi yote ya wabunge yakishaapishwa wote ni wabunge wanaofanana katika hadhi ya kufanya kazi wanapokuwa Bungeni.
“Katiba ilivyoyaweka makundi
matano ya wabunge kuanzia wanaoteuliwa na Rais, wanaochaguliwa na
wananchi, wabunge wa viti maalumu na wanaotoka Baraza la Wawakilishi
Zanzibar na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wote wamewekwa kwa sababu
maalumu kwa sababu hiyo wabunge wote ni sawa” Amesema Dkt. Tulia
Aidha Naibu Spika
ameitaka jamii kubadilika kutoka katika dhana kwamba mwanamke ambaye
anashika nafasi ya juu katika uongozi kwamba amebebwa.
“Wanawake wengi ambao
wamepewa nafasi ya uongozi kwa kuchaguliwa au kuteuliwa ni mara chache
sana hufanya vibaya na hata akifanya vibaya jamii humhukumu kwa kuwa ni
mwanamke wakati kuna wanaume katika nafasi kama hiyo ambao pia unakuta
wamefanya vibaya hivyo kuna changamoto hiyo katika jamii” Amesema Naibu
Spika Dkt. Tulia.
Kwa upande mwingine
Naibu Spika Dkt. Tulia amesema anaongoza Bunge bila upendeleo wowote ila
anafuata sheria na kanuni za kuongoza Bunge.
0 comments:
Post a Comment