Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akielezea namna matumizi ya vifaa vya Kielektroniki (EFDs) yalivyoongeza Makusanyo ya Mapato ya Serikali alipotembelewa na Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), Ofsini kwake jijini Dar es salaam.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), akielezea nia ya Benki yake ya kutaka kuwekeza kartika Sekta ya Kilimo, alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani) ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akichukua maelezo ya Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), baada ya ya Mtendaji huyo kumtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam na kueleza nia ya kuzitumia fursa zilizopo katika Sekta ya Kilimo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akifafanua jambo kuhusu uwekezaji katika Sekta ya Kilimo unaotaka kufanywa na Benki ya UBL Nchini Tanzania baada ya kukutana na Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Faisal Aliza Jamall OfIsini kwake jijini Dr es salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
Benki
ya UBL imesema iko tayari kuwekeza Tanzania katika Sekta ya Kilimo
ambayo itawezesha Tanzania kupata fursa ya kuweza kuuza mazao yake
katika nchi za ughaibuni na pia kufanya kazi na Watanzania pamoja na
Serikali yake.
Hayo
yalisemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Tanzania, Bw. Faisal
Jamall wakati akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb), ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Bw.
Jamall alisema kuwa kwa sasa Tanzania inaenda vizuri hasa katika suala
la ukuaji wa uchumi ingawa kuna baadhi ya wananchi wanalalamika kuwa
fedha zimeadimika mitaani lakini ni wazi kwamba Taifa linarudi kwenye
utaratibu. Hivyo wameonesha nia ya kuwekeza hasa katika Sekta ya Kilimo.
Naye
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) amesema kuwa
hali inabadilika na Jumuiya ya Mabenki inaanza kuwa na imani na
Tanzania. Na kuongeza kuwa kitendo cha Benki ya UBL kuonesha nia ya
kufanya kazi na Serikali katika Sekta ya Kilimo ni jambo jema katika
maendeleo ya haraka ya Tanzania kwa kuwa Sekta hii mama bado inakabiliwa
na changamoto nyingi.
Alisema
dhamira kubwa ya Benki ya UBL ni kuwekeza katika kilimo cha
umwagiliaji, uboreshaji wa mifugo pamoja na uvuvi. Na Serikali imeahidi
kuitumia vizuri fursa hii ili nchi iweze kupiga hatua ya haraka zaidi
hasa katika kipindi ambacho imedhamiria kuwa nchi ya Viwanda.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu matumizi ya dola katika uchumi badala ya shilingi ya
Tanzania, hasa kwenye mikopo, Waziri Mpango alisema kuwa suala hili
Serikali imeshaanza kulifanyia kazi kwa kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja
na kusimamia kwa karibu biashara ya maduka ya fedha za kigeni.
“Tumepiga
hatua ya kufunga mashine za kielektroniki (EFDs) ili Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) kuona kinachofanyika ili wamiliki wa maduka hayo walipe
kodi inayostahili. Aidha zoezi hili litaweizesha Benki Kuu ya Tanzania –
BoT, kuona kiasi cha fedha za kigeni zilizopita katika maduka na
itaimarisha matumizi ya shilingi ya Tanzania; japo tuna changamoto kubwa
ya wananchi kutokudai risiti pindi wanapopata huduma ya kubadilisha
fedha za kigeni,” Alisisitiza Dkt. Mpango.
Katika
kuhitimisha majadiliano hayo Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.
Mpango alisema Serikali itaongeza ushirikiano na Benki ya UBL ili waweze
kufanya biashara, ikizingatiwa kuwa Benki hiyo ni miongoni mwa Benki
kubwa katika nchi za Uarabuni.
Imetolewa na:
Kitengo na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
16 Februari, 2017
0 comments:
Post a Comment