Home » » TANZANIA YAWA NCHI YA KWANZA KUSIGN MAKUBALIANO YA MWONGOZO NA KANUNI ZA UONGOZI KWA WAMILIKI NA MAMENEJA WA VYOMBO VYA HABARI..

TANZANIA YAWA NCHI YA KWANZA KUSIGN MAKUBALIANO YA MWONGOZO NA KANUNI ZA UONGOZI KWA WAMILIKI NA MAMENEJA WA VYOMBO VYA HABARI..

:
Waziri Nchimbi akiweka saini makubaliano hayo na Mwenyekiti wa Moat, Reginald Mengi (kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya kuendeleza Vyombo vya Habari Afrika (AMI), Amadou Mahtar Ba.
---
TANZANIA imekuwa nchi ya kwanza Afrika kusaini makubaliano ya mwongozo na kanuni za uongozi kwa wamiliki na mameneja wa vyombo vya habari.

Mwongozo huo ulisainiwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT) Reginald Mengi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Mpango wa Vyombo vya Habari (AMI) Amadouh Mahtar Ba.

Kwa mujibu wa Mengi, lengo la mwongozo huo ni kujenga tasnia ya habari yenye kuzingatia maadili katika maeneo ya utawala, uwazi na uaminifu bila kuingiliwa na ushawishi wa mtu yeyote.

Alisema kumekuwa na wimbo wa maadili ya wanahabari pekee na kusahau suala zima la wamiliki ambao nao wakati mwingine huchangia kwa kiasi kikubwa habari kuandikwa ay kurushwa hewani zikiwa na mapungufu ya kimaadili.

Naye Amadouh alisema kwa mara ya kwanza duniani, kikundi cha wanataaluma ya habari Afrika kimekutana na kuja na mpango wa kuweka suala la mwongozo na maadili kwa wamiliki na mameneja wa vyombo vya habari.

Aidha Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Dk Emmanuel Nchimbi wakati akizindua mwongozo huo, alisema kwa upande wa Serikali inapongeza mwongozo huo na ina imani utekelezaji wake utafanyika kwa ufanisi kwa kuwa watekelezaji wake wakuu ndio waanzishili.

Baadhi ya wadau wa habari waliochangia maoni yao katika mkutano huo ni pamoja na mwanahabari mwandamizi na mmoja wa wamiliki wa vyombo vya habari nchini, Jenerali Ulimwengu, Profesa Palamagamba Kabudi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Kaimu Mhariri Mkuu wa kampuni ya Tanzania Standard Newspapers (TSN) Mkumbwa Ally.




0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa