Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » SUPER D AENDELEA KUTOA MAFUNZO YA MCHEZO WA MASUMBWI BURE KWA VIJANA

SUPER D AENDELEA KUTOA MAFUNZO YA MCHEZO WA MASUMBWI BURE KWA VIJANA


Kocha wa Mchezo wa Masumbwi hapa nchini,Rajabu Mhamila 'Super D'  (kushoto) akimwelekeza mmoja wa vijana waliojitokeza katika mafunzo ya mchezo wa masumbwi, Roger Msami jinsi ya kumdhohofisha mpinzani wakati wa mchezo kwa kupangua ngumi zake kwa kiwiko wakati wa mazoezi yaliyofanyika kwenye ufukwe wa GYKHANA jijini Dar es salaam jana.
Kocha wa Mchezo wa Masumbwi hapa nchini,Rajabu Mhamila 'Super D' (kushoto) akimwelekeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' jinsi yakupangua ngumi za mpinzani wakati wa mazoezi yaliyofanyika kwenye ufukwe wa GYKHANA jijini Dar es salaam jana.
Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' (kushoto) akimwelekeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' jinsi kupiga ngumi za tumbo huku akiwa ameingia ndani kwa mashambulizi zaidi wakati wa mazoezi yaliyofanyika kwenye ufukwe wa GYKHANA jijini Dar es salaam jana.
Kocha Rajabu Mhamila 'Super D'  akionyesha umahiri wake wa kurusha masumbwi wakati akiwaelekeza vijana waliojitokeza katika mazoezi jinsi ya kupiga ngumi za tumbo na kuingia ndani kwa mashambulizi zaidi.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa