president-barack-obama
Rais wa Marekani, Mhe. Barack Obama anatarajiwa kuwasili nchini  leo tarehe 01 Julai, 2013 mchana kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam, Mhe. Rais Obama ambaye atafuatana na Mkewe Mama Michelle atapokelewa na Mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.Baada ya mapokezi, Mhe. Rais Obama atakwenda Ikulu kwa mazungumzo rasmi na Rais Mhe. Kikwete. 
 
Aidha, atafanya mkutano na Wafanyabiashara na kuhudhuria Dhifa ya Kitaifa.Tarehe 2 Julai 2013, Mhe. Rais Obama atatembelea Mitambo ya kufua Umeme ya Symbion iliyopo Ubungo, Dar es Salaam na kuzindua rasmi Mpango Maalum wa Maendeleo ya Nishati Barani Afrika ulioanzishwa na  
 
Marekani (Power Africa Initiative).Mpango huo utaanza na nchi saba ambazo ni: – Tanzania, Kenya, Uganda, Ethiopia, Ghana, Nigeria na Sudan Kusini.Mhe. Rais Obama anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 02 Julai 2013.IMETOLEWA NA:
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM
30 JUNI, 2013
 
Monday, July 1, 2013
-On Monday afternoon, President Obama takes part in a formal arrival ceremony in Dar es Salaam, Tanzania.
-President Obama participates in a bilateral meeting and joint press conference with President Jakaya Kikwete of Tanzania.
-In the evening, President Obama participates in a CEO roundtable and business leaders forum.
-President Obama and President Jakaya Kikwete of Tanzania participate in an official dinner.

Tuesday, July 2, 2013
-On Tuesday morning, President Obama takes place in a Consulate meet and greet.
-President Obama visits the Ubungo Power Plant.
 
Atakapowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere na ndege yake  Air Force One, Rais w Maekani, Barack Obama atazindua barabara mpya upande wa Mashariki wa lango la kuingia Ikulu ambayo inatarajiwa kuitwa Barack Obama.Baada ya shughuli hiyo atazungumza kwa nyakati tofauti na wafanyabiashara wa nchi za Afrika na Marekani kwenye hoteli ya Hyatt Regency,  Dar es Salaam.  
 
Amepanga pia kuzungumza na maofisa wa Ubalozi wa Marekani nchini.Baadaye atahudhuria dhifa ya taifa usiku ambayo imeandaliwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam.Kesho ataweka shada la maua sehemu ulipokuwa Ubalozi wa Marekani ikiwa ni kumbukumbu ya watu waliouawa katika shambulizi la kigaidi la bomu mwaka 1998, Dar es Salaam. Pia atatembelea mitambo ya kufua umeme ya kampuni ya Symbion iliyoko Ubungo.
Rais Obama atatoa hotuba kuzungumzia mikakati ya Marekani ya kusaidia Afrika kuzalisha nishati ya umeme.
Michelle atakuwa na ratiba yake ambapo atapata staftahi na mwenyeji wake, Salma Kikwete katika ofisi za Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), Dar es Salaam.
Pia atatembelea sehemu ulikokuwa ubalozi wa Marekani na kisha atashuhudia onesho la utamaduni la kikundi cha Baba wa Watoto, ambacho kinajumuisha watoto wa mitaani wenye umri wa kuanzia miaka mitano hadi 18 kwenye Makumbusho ya Taifa.
Jumanne, Michelle atahudhuria mkutano na wake wa marais wa nchi za Afrika ambao pia utahudhuriwa na mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush, Laura.
Julai 2, Rais Obama atatembelea mitambo ya kufua umeme ya Symbion Ubungo saa 4 asubuhi na kisha msafara wake utapita Nelson Mandela, Tazara hadi uwanja wa ndege na kuondoka saa 5.20 asubuhi. 

Obama ametangaza mpango wa kuwajengea uwezo viongozi vijana wa Afrika kwa kuwapa mafunzo ya uongozi katika vyuo vikuu vya Marekani hasa katika masuala ya utawala, biashara na uongozi.
Katika hotuba yake katika Chuo Kikuu cha Johannesburg juzi jioni, alisema hatma ya Afrika iko mikononi mwa vijana; hivyo ni lazima wawezeshwe ili kuliongoza vizuri bara hili.
Alisema mafunzo hayo yatatolewa  chini ya mpango wa ufadhili wa Marekani kwa viongozi vijana ambao utawajengea uwezo wa kuendesha huduma za kiserikali ikiwa ni pamoja na biashara na   kuhudumia jamii yao.
Kuanzia mwaka ujao Marekani itatoa mafunzo kwa vijana 500 ambayo yatakuwa ya wiki sita ambapo idadi hiyo itaongezeka hadi vijana 1,000 kila mwaka.
Watakaofadika ni vijana wa kati ya umri wa miaka 25 hadi 35 ambao wamekuwa wakijihusisha na uongozi  ndani ya Serikali, sekta binafsi na asasi za kiraia. Alisema washiriki hao ni lazima waoneshe dhamira yao katika kuitumikia jamii.
Obama alisema Afrika ina mwonekano mzuri kwa siku zijazo na kuwataka vijana wa Afrika kuhakikisha wanatumia uwezo wao katika kutumikia bara lao.
Mpango wa kuendeleza vijana wa Afrika ujulikanao kama YALI ulizinduliwa mwaka 2010 na Rais Obama ikiwa ni sehemu ya kusaidia maendeleo, kuhamasisha ujasiriamali na kujenga uwezo wa Afrika kuwa na viongozi bora wa kizazi kijacho.