Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » MAONYESHO YA NYUMBA NA VIFAA VYA UJENZI MLIMANI CITY YAVUTIA WENGI

MAONYESHO YA NYUMBA NA VIFAA VYA UJENZI MLIMANI CITY YAVUTIA WENGI

 Hiki ni Kifaa ambacho Kinatumia Mionzi ya Jua kwa Ajili ya Kuchemsha Maji ni Kifaa cha Kisasa kabisa kutoka Ensoi ambao ndio wanazalisha bidhaa hii.
 Huyu ni Muelimishaji ambaye kwa hakika kazi yake ilipendwa na watu wengi na kuhamasika kununua vifaa mbalimbali vilivyo tenngenezwa na Ensol wakati wa Maonesho Ndani ya Mlimani City . Hapa alikuwa akitoa Maelezo ya kina juu ya Jinsi Kifaa kinacho tumia Mionzi ya Jua Kinavyo weza Chemsha maji.
 Banda hili la Ensol likiwa Linamelemeta kwa sana huku kila mtu akihamasika kutembelea

Hili ni Banda la Camel Cement na Camel Gas, kwa hakika kiwanda hiki cha kutengeneza Cement kipo makini na wanatengeneza Cement Bora kabisa ambayo kila mtu anashauriwa kwenda kununua wakati wa ujenzi
 Watu wengi walivutiwa na Banda hili ambalo walishuhudia jinsi aina mbalimbali ya Madirisha yanavyo tengenezwa na kujionea aina hizo ambazo kwa ukweli kama ukiweka katika nyumba yako hakika itakuwa inapendeza mpaka mwisho.
 Hapa ni NOELA GEN SUPPLY wasambazaji wa vifaa mbalimbali vya kumalizia ujenzi katika nyumba yako hasa Jakuzi kama linavyo onekana hapa ni La kisasa kabisa ambalo kwa hakika ukiingia kuoga unaweza pitiliza na kulala hapo hapo, Jakuzi hili lina eneo la kupumzikia , Masaji na kila kitu .
 Baadhi ya Vitu zaidi ndani ya banda la Noela

 Eneo hili ni la Muhimu sana hawa wanaitwa OPEN SANIT kwa ukweli watu hawa wamekuwa ni Tishio sana na wanaongoza kwa kuuza kwa bei nafuu kabisa vile vifaa vyote vya kuvaa katika lindo lakini pia zaidi kwa vifaa vya kukufanya uwe salama wakati wa ujenzi , Watoa maelezo makini walikuwepo eneo hilo kutoa elimu ya Bure na kuwashauri watu juu ya umuhimu wa vifaa hivyo.
 Hakuweza kupatikana Jina lake kwa Mara Moja Mwanadada huyu Mahili ambaye alitoa maelezo ya kina sana kuhusiana na INVERTER  ya kisasa kabisa ambayo kwanza yenyewe ni automatic na inaunganishwa moja kwa moja katika umeme wa Luku, INVERTER hiyo ambayo ni ya kisasa zaidi inauwezo wa kukaa hadi masaa 12 baada ya umeme kukatika huku Mtumiaji ukifuarahia huduma zako zote kama kutazama TV, Kunyosha Nguo zako na mambo Mengine mengi sana.   hata hivyo INVERTER zipo za aina nyingi unaweza chagua ukubwa unao hitaji kulingana na matumizi yako. karibu sana hapa CHLORIDE EXIDE
 INVERTER ya kisasa kama inavyo onekana hapa , bado haujachelewa wahi sasa upate yako.
 Baadhi ya wadau wakipata maelezo ya kina juu ya vitu mbali mbali vinavyo patikana CHLORIDE EXIDE
 Hawa Ni Wataalam kabisa wa mambo ya Masoko yani kwa Lugha ya Kigeni wanaitwa (MARKETERS) na kampuni yao inakwenda kwa jina la Prime Location , wanahusika na mambo ya matangazo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwasaidia watu kutangaza Biashara zao kupitia Barua pepe yaani Bulk Emails , Kutumia njia ya Ujumbe mfupi wa Maneno yaani Bulk SMS na pia wanatumia Njia ya Magazine ambayo inapatikana kila kona ya Super market na Shopping Malls kubwa mteja unaweza jitangaza hapo kwa Bei nafuu kabisa.

Pichani ni Mshauri katika upande wa Masoko akitoa maelezo ya kina umuhimu na Faida za kutangaza nao ikiwa ni sehemu ya kukuza Biashara

 Hapa Baadhi ya Wadau wakiwa wanapata maelezo

 Watengenezaji wa Mabati makini kabisa na ya kisasa wanao kwenda kwa Jina la NABAKI AFRIKA pia wanatengeneza na kuuza vifaa mbalimbali vya majumbani ikiwemo Solar Power kwaajili ya kuchemshia maji, Water Filter na vingine vingi .
 Ukiangalia Picha kwa Umakini mkubwa inajieleza yenyewe hapa, Hawa ni wataalam wa kukandalia wewe Sherehe, pia ni wataalam kabisa wa kutengeneza Kadi kulingana na matakwa yako wanakwenda kwa jina la FANTASTIC CARDS usiache watumia kama una kazi.
 Wanaitwa See Breeze
 Shirika la Nyumba la NHC
 Banda la TRA


 Banda la Mfuko wa Pensheni wa PSPF walikuwepo wakionesha Nyumba zao 

Wanaitwa Mr. Quality wauzaji wa Mabati ya kisasa na Milango ya kisasa , Mabati yao yana Garantii ya Miaka 30 , usipoteze muda wako wahi sasa Kamata Fursa nunua mabati yao kwa ujenzi Bora
 Maonesho haya yameisha Leo..

Picha zote na Blogs za Mikoa  kupitia Mtandao wa Dar es salaam Yetu

1 comments:

Unknown said...

you sharing very good infomratiom. I like your post.

Thank you.

Clear Water Filters

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa