Idara
ya Uhamiaji nchini imewakamata raia wanane wa kigeni (pichani chini)
wakati wakiingia nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu
Nyerere wakiwa na pasipoti bandia za kusafiria za Mataifa tofauti ya
Ulaya.
Wageni
hao walikuwa wakijaribu kuingia nchini leo tarehe 15.08.2014 majira ya
saa nane na nusu usiku kwa ndege ya shirika la ndege la Uturuki yenye
Namba TK 603, wakitokea Uturuki na kujitambulisha kuwa ni raia wa
Sweden na Belgium.
Maofisa Uhamiaji katika kituo hicho baada ya kuwatilia mashaka na
kuwafanyia ukaguzi wa kina, waligundua kuwa wageni hao ni Raia wa Iraq
wakijaribu kuingia nchini Tanzania na pasipoti za bandia.
Kukamatwa
kwa wageni hao ni jitihada za Idara ya Uhamiaji kupambana na Uhamiaji
haramu nchini ambapo suala la zima la udhibiti wa mipaka linapewa
kipaumbele.
Akizungumzia tukio
hilo, Kaimu Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Tatu Burhan, anasema, kwa
kutumia ujuzi na weledi walionao Maofisa Uhamiaji wanaendelea
kufanyakazi usiku na machana kuhakikisha Sheria na Taratibu za Uhamiaji
zinafuatwa.
"Idara
ya Uhamiaji, iko macho hatulali ili kuhakikisha ulinzi na usalama wa
nchi ikiwa ndio jukumu letu namba moja unaimarika. kwahivyo, kila
mtu awe raia wa kigeni na Watanzania wanapaswa kufuata Sheria na
Taratibu zilizopo za kuingia na kutoka nchini"
Hadi sasa, Wageni hao wamezuiliwa kuingia nchini na wanaendelea
kushikiliwa na Maofisa wa Idara ya Uhamiaji kituoni hapo huku wakisubiri
kurudishwa walikotoka.
Hili
ni wimbi lilioibuika hivi karibuni kwa baadhi ya raia wa nchi za Iraq,
Iran, Syria kujaribu kuingia nchini isivyo halali huku ikisemekana lengo
lao kubwa ni kuingia Tanzania na baadae kutoka kuelekea mataifa ya
Ulaya.
Majina
ya Wageni hao na Pasipoti bandia walizokuwa wakitumia pamoja na Majina
halisi na Pasipoti zao za Iraq zilizogunduliwa baada ya upekuzi kwenye
mabano ni kama ifuatavyo;
1. ADEL SHAALAN MOHAN - SWEDISH, PPT. NO. EI282207 ( ADEL SHAALAN MOHAN Pasipoti Nam. G1489664)
2. SAMER HELMI KAMIT - SWEDISH, PPT. NO. 87187804 ( LAZIM MOSA HITEET, PPT. Namba, A 13466001)
3. MOHAMMED JAFAR AL MOSAWI - SWEDISH, PPT.NO. 87168871 (ALI HUSSEIN OLEIWI, PPT. NO. G 1111623)
4. DAVID GABRIEL POBLETE - SWEDISH PPT.NO. 86867751 (AYAD SAMI MAKTTOOF, PPT NO. A 4910203)
5. SADDAM ALKHAMERI AREF - SWEDISH, PPT NO. 81640513 (SAIF ALDAN FALIH HASAN, PPT. NO. G 1489664)
6. ALI MOHAMMED ABDULLAH - IRAQ, PPT. NO. A 5931725
7. OSAMAH ZAID GHAEB AL-OBAIDI - IRAQ, PPT. NO. A 6175951
8. ALI HUSSEIN OLEIWI - IRAQ, PPT. NO. G 1111623
1 comments:
Wasije wakawa wana-connection na mitandao ya kigaidi pia hao
Post a Comment