Mkuu wa Bregedi ya Nyuki ambae ni Makamo Mwenyekiti wa michezo ya
Majeshi Bregedia Jenerali Sharif Sheikh Othman akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu michezo ya nane ya Majeshi ya Jumuia ya Afrika Mashariki. Mkuta
huo umefanyika huko Bregedi ya Nyuki Migombani Zanzibar.
Mkurugenzi wa ufundi wa mashindano hayo upande (JWTZ) Luteni Kanali Joseph Bakari akitoa ufafanuzi wa Michezo hiyo.
========== ==========
Na Miza
Othman Makame Maelezo- Zanzibar .
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein
anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Michezo ya nane ya Majeshi ya
Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki itafanyika Zanzibar kuanzia tarehe 18
mwezi huu.
Akitoa
Taarifa ya Mkuu wa Majeshi ya Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Makao Mkuu ya Brigedi Migombani kwa waandishi
wa Habari, Mkuu wa Brigedi hiyo Brigedia Jenerali Sharif Sheikh Othman amesema
lengo la michezo hiyo ni kujenga mashirikiano kati ya Majeshi na Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Amesema
katika Michezo hiyo kutakuwa hakuna mshindi wala aliyeshindwa na wote watakuwa
washindi, lengo ni kujenga uweledi na nidhamu ndani ya majeshi yetu.
“Hii ni
fursa ya wanajeshi wetu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kukutana pamoja kama
tunavyofanya katika mazoezi ya pamoja ya kijeshi”, alisema Brigedia Jenerali
Sharif Sheikh Othman.
Amezitaja Nchi
za Jumuiya hiyo zitakazoshiriki Michezo
hiyo kuwa ni wenyeji Tanzania, Burundi, Rwanda, Kenya na Uganda. Amesema Michezo itakayochezwa na wanajeshi hao
ni Mpira wa Miguu, Mpira wa Pete, Mpira
wa Mikono, Mpira wa Kikapu na Mbio za
nyika na ameelezea viwanja
vitakavyofanyika kwa ajili ya michezo hiyo
Polisi ziwani ,Vyuo vya Mfunzo Kilimani, JKU Saateni, Pamoja na Viwanja
vya Zimamoto na Uokozi.
Brigedia
Jenerali Sharif Sheikh ambaye pia ni Makamo
Mwenyekiti wa Michezo hiyo, amewataka
Wananchi kujitokeza kwa wingi katika kuona vipaji vitakavyoonyeshwa na
wanajeshi kutoka Nchi hizo .
0 comments:
Post a Comment