Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » Balozi wa kutetea watoto waishio mazingira magumu aiomba Serikali kuwaangalia watoto hao kwa jicho la tatu

Balozi wa kutetea watoto waishio mazingira magumu aiomba Serikali kuwaangalia watoto hao kwa jicho la tatu

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Na Lilian Lundo - Maelezo

Msanii wa Filamu na Balozi wa kutetea watoto waishio katika mazingira magumu Salma Jabu (Nisha) ameiomba Serikali kuwaangalia watoto hao kwa jicho la tatu.

Nisha aliyasema hayo wakati akikabidhiwa ubalozi wa kudumu wa kutetea watoto waishio mazingira magumu wa New Hope Family Group leo jijini Dar es Salaam.

“Watoto hawa wamekuwa rafiki zangu kwa muda mrefu, nimekuwa na huruma sana pale nilipowaona wanalala na njaa wakati watoto wengine wanakula na kusaza,” alisema Nisha.

Nisha aliongeza kwa kusema ni wakati wa kuwafuta machozi na wao wajione ni moja ya jamii ya kitanzania, kwa yoyote mwenye nguo tatu basi nguo moja atoe kwa ajili ya watoto hao.

Pia muigizaji huyo ameiomba Serikali kuangalia watoto hao kwa jicho kubwa, kwani yapo mengi ambayo wanahitaji ikiwa pamoja na elimu ili waweze kujiepusha na makundi mabaya ya mitaani.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa New Hope Family Omary Kombe alisema si jambo la busara kumwita mtoto majina kama panya rodi na mbwa mwitu huku tukihubiri amani na upendo kwenye majukwaa ya siasa na nyumba za ibada.

Aidha, Kombe amesema kuwa, familia ya New Hope imemchagua Nisha kuwa Balozi wao kutokana na moyo wake wa upendo na huruma si tu kwa watoto waishio katika mazingira magumu bali kwa jamii ya watu maskini na wanyonge.
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa